Loading...

MFANYABIASHARA AKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO SONGEA


MFANYABIASHARA AKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO SONGEA
Picha ya kiganja haihusiani na habari
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu watatu wa familia mmoja wakazi wa eneo la Ruvuma chini lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kukutwa na kiganja cha binadam ambacho kimekutwa ndani ya duka la linalomilikiwa na familia hao.


Habari zilizopatikana jana ambazo zimezibitishwa na kaimu kamanda wa mkoa wa Ruvuma George Chiposi zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea February16 mwaka huu saa za mchana huko katika eneo la Ruvuma chini nje kidogo na Manispaa ya Songea.


Kaimu kamanda wa polisi Chiposi amewataja wanaoshikiriwa kuwa ni Denis Kalsinje (42) ambaye ni mfanya biashara na ni mkazi wa eneo la Ruvuma chini, Sabina Hakika (38) maarufu kwa jina la Mduma ambaye ni mke waDenis Kalsinje na Emmanuel Kalsinje (36) ambaye ni mdogo wa Denis Kalsinje.

Chiposi alimwambia mwandishi wetu jana mchana ofisini kwake kuwa polisi ilipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kunamfanyabiashara mmoja huko katika eneo la Ruvuma chini anafanya biashara sana kwa vile ameweka kiganja cha binadam kwenye duka lake ambacho inadaiwa kuwa ndicho kinachokuwa kinavuta wateja taarifa ambayo polisi ilifanyia kazi kikamilifu.


Alisema kuwa February 16 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi mkaguzi msaidizi wa polisi Karimu Mtikula akiwa na askari polisi wenzake waliondoka wakitokea ofisi ya Mkuu wa upelelezi ya makosaya jinai mkoa wa Ruvuma walienda hadi kwenye eneo la Ruvuma chini ambako walifika kwenye eneo la tukio na kufanya upekuzi wa kina ndani ya duka la mfanya biashara huyo Denis na kufanikiwa kukipata kiganja kimoja cha mkono wa kushoto wa binadam.


Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa kiganja hicho kilikutwa kimehifadhiwa kwenye kasha la kuhifadhia marashi ambalo liliandikwa Blue For man na kuviringishwa kwenye mifuko mitatu ya Rambolikiwa ndani ya duka la mfanya biashara huyo.


Hatahivyo Kaimu kamanda Chiposi alisema kuwa katika mahojiano ya awali mfanyabiashara huyo Kalsinje alikili kukutwa na kiganja cha binadam kwenye duka lake lakini anashindwa kuelewa ni nani aliye kileta na kukiweka ndani ya duka lake.


Alieleza kuwa katika tukio hilo watuhumiwa hao wamesha kamatwa na kwamba kwa sasa hivi polisi inaendelea kufanya upelelezi zaidi wa tuki hilo na ukikamilika watuhumiwa watapelekwa mahakamani kujibu mashitaka yao yanayo wakabili



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top