MTAMBO mmoja wa kufulia umeme kati ya mitambo mitambo ya shirika la
umeme Tanzania (Tanesco) mkoani Ruvuma umedaiwa kuwa na itilafu na
kusababisha kuwepo na mgao mklai wa umeme katika halmashauri ya manispaa
ya Songea na vitongoji vyake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano
wa maliasili wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Meneja wa Tanesco mkoani
humo Mhandisi Monika Kebara alisema kuwa mtambo ambao umeharibika ni
ule aliokuwa ameuleta raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Kikwete katika ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni za
uchaguzi mwaka juzi mjini Songea.
Alisema kuwa mtambo huo wa kufulia umeme wa megawati 1.9 ulianza
kukorofisha toka wiki iliyopita hivyo kusababisha kuwepo kwa upungufu
mkubwa wa upatikanaji wa umeme katika manispaa ya Songea kwani awali
kabla ya kuharibika kwa mtambo huo umeme ulikuwa unazalishwa megawati
4.6 kwa mashine zote tano.
"Hata hivyo naomba niwaweke wazi kuwa tatizo hili hatawahusu wale
wote ambao wapo katika maeneo muhimu kama vile hospitali na baadhi ya
maeneo ya makambi ya jeshi na mjini kati kutokana na unyeti wa shughuli
zake.
Aidha alisema kuwa hawezi kusema kuwa tatizo hilo litakwisha lini
kwani mafundi wako kazini wakiwa wanafanyia matengenezo mtambo huo
ambao ndio tegemeo kubwa kwa kufua umeme katika halmashauri ya manispaa
ya Songea na vitongoji vyake.
Hata hivyo baadhi ya waandishi wa habari walimtaka meneja huyo wa
Tanesco Mhandisi Kebara ahakikishe kuwa anakuwa makini katika
kuwasimamia mafundi waliofika kufanyia matengenezo matambo huo na
wamemtaka awe makini katika kuhakikisha kuwa wananchi wa manispaa hiyo
wanapata umeme wa mgao bila kuwepo a upendeleo wa baadhi ya mameneo.
Post a Comment