MAHAKAMA ya hakimu mkazi Mkoa wa Ruvuma imewahukumu raia
kumi na sita wa Nchi ya Ethiopia kulipa faini
ya Sh. 50,000 kila mmoja au kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja baada ya
kutiwa hatiani kwa kosa la kuingia nchini bila ya kuwa na vibali ambapo
wameshindwa kulipa faini na wamepelekwa gerezani kuanza kutumikia kifungo cha
miezi kumi na mbili.
Hakimu mkazi wa
mahakama hiyo Casmili Mwarunyungu akisoma hukumu hiyo alisema kuwa
washtakiwa kwa vile wamekiri wenyewe kosa mahakamani hivyo mahakama inawapa
adhabu ya kulipa faini ya sh.50,000 au
kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja .
Kwa upande wake mwendesha mashtaka toka ofisi ya idara ya
uhamiaji Greta Banda alidai mahakamani hapo kuwa Yeremias Aremu na wenzake kumi
na tano ambao ni raia wa Nchi ya Ethiopia inadaiwa Januari 25 mwaka huu majira
ya saa 4 usiku huko katika eneo la kijiji cha Mtyangimbole kwa pamoja
walikamatwa na askari wa polisi ambao warishirikiana na maafisa uhamiaji bila
kuwa na vibali vinavyowaruhusu kuwepo katika Nchi ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa mara ya
kwanza walifikishwa mahakamani Januari 29 mwaka huu ambapo mwendesha mashtaka
toka Idara ya Uhamiaji Greta Banda aliiomba mahakama hiyo kuhairisha kesi hiyo
kutokana na kutokuwepo mkalimani wa kutafsiri lugha ya ARMARIC ambayo ndio
inayotumika Nchini Ethiopiakwa kutafsiri katika lugha ya Kiswahili.
Alieleza zaidi mahakamani hapo kuwa mtaalam wa kutafsiri
lugha hiyo alikuwa ameandaliwa kufika mahakamani Januari 30 mwaka huu toka
shule ya sekondari ya De Poul l iliyopo katika manispaa ya Songea hivyo
mahakama ilikubali ombi la mwendesha mashtaka kisha kesi hiyo iliahirishwa na
kuletwa tena mahakamani jana (leo).
Washttakiwa wote kwa pamoja baada ya kusomewa shitaka lao
warikili kosa na kukubaliana na maelezo ya shitaka yaliyosomwa na mwendesha
mashtaka toka idara ya uhamiaji Banda hivyo mahakama iliwatia hatiani kama
walivyoshitakiwa na kuwahamuru walipe faini y ash. 50,000 kila mmoja au
kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kila mmoja na wote wameshindwa kutimiza
sharti la kulipa faini.
Post a Comment