Loading...

WALEMAVU WA KUTOSIKIA MKOANI RUVUMA WATOA MAONI YA KATIBA MPYA WAOMBA KERO ZAO ZIWEKWE BAYANA NDANI YA KATIBA MPYA


WATU  wenye ulemavu wa kuto sikia  Mkoani  Ruvuma wametoa mapendekezo yao  kuwa katiba mpya  ni vyema  iweke bayana  lugha kwa watu wenye ulemavu  wa kuto sikia  na  wamependekeza  uwepo mgawanyo wa madaraka  mfano, wabunge wasiteuliwe kuwa  mawaziri  na Wakuu wa Mikoa  wasichaguliwe  kuwa   wabunge  kwani  Jamhuri  ya  Muungano wa Tanzania   ina  wasomi wengi.

Hayo yamesemwa jana  kwenye  semina  ya Chama  Cha  Viziwi  Tanzania
( CHAVITA)  mkoani  Ruvuma  ya kuwajengea  uwezo  wa namna ya kutoa maoni ya katiba  mpya  iliyofanyika kwenye  ukumbi wa mikutano  wa chama cha  Ushirika  wa kuweka  na kukopa  cha Halmashauri  ya  wafanyakazi wa  manispaa  ya  Songea.

Katika  semina  hiyo  iliyofadhiliwa  na  THE  FOUNDATION  OF  CIVIL  SOCIETY  ORGANIZATION  ya  jijini  Dar  es  Salaam   Hery   Chaima  mjumbe  wa  Chama Cha  Viziwi  Tanzania  mkoa  wa Ruvuma  alisema  kuwa  anapendekeza  kuwa  katiba  mpya   ni vyema  Rais  apunguziwe madaraka  kwani   sio  lazima  wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya,  Miji, Manispaa  na  Majiji  wateuliwe  na Rais  na badala  yake  uteuzi  ufanywe  na  waziri  mkuu.

Chaima  alisema  kuwa  kufanya  hivyo Rais  kutampunguzia  kazi zake  za kila  siku na  ameiomba  katiba  mpya  iweke  bayana  lugha  kwa watu wenye ulemavu  wa kuto sikia  na  kwamba  makundi maalumu  serikali  yatambue  kama ni makundi  yanayo hitaji  kutoa  maoni  kama  watu  wengine  na  iyasamini    na  kuyajali  kama  wao ni binadamu kama  wengine.


Kwa  upande  wake  mtaalamu  wa  lugha  alama  Mery  Haule  alisema  kuwa  walemavu  wasiosikia   wanahitaji  kupata  msaada  mkubwa  kwa jamii  hivyo katiba  mpya  ni vyema  iwatambue  pale  wanapopata  matatizo  ya  ugonjwa  Hospitalini waweze  kusaidiwa kwa  uraisi vilevile  wanapopatwa na matatizo kwenye vituo vya  polisi, mahakamani na  sehemu  zingine  wanatakiwa wawepo  wataalamu  wa lugha  alama  wa   kuwasaidia  kwani kwa hivi sasa wamekuwa wakipata shida  pale matatizo  yanapotokea.

Naye  Abdul  Homera  mkalimani wa lugha  alama  Tanzania  ameiomba  serikali   ione  umuhimu wa  kutoa  upendeleo  kwa  walemavu  wasiosikia   na  walemavu  wengine  kwa  kuwapa  ajira  kwani  hali zao  kimaisha  ni ngumu.

Alifafanua  zaidi kuwa  wakalimani  wa l ugha  alama  vile vile watambulike  ndani ya katiba mpya  nalugha ya alama  itambulike kama lugha rasmi ya Taifa  na  mkalimani wa lugha  alama  kwanza ni vyema alipwe au  ahajiliwe  na  serikali kama wanataaluma  wengine wanavyopatiwa ajira na serikali.

Homera  aliiomba  serikali hichukue hatua  za makusudi  za  kujengwa kwa vyuo  vya  lugha  alama maana  hapa nchini  hakuna  hata chuo  kimoja  ambacho  kinafundisha taaluma  hiyo.

Mwenyekiti  wa Chama  cha  Viziwi Tanzania  (CHAVITA)  mkoa  wa  Ruvuma  Kelvin  Vicent   amesema  kwenye  katiba  mpya  ni  nyema  mgombea  binafsi wakati  wa  kumchagua  raisi  awepo  ili  kuweka  bayana  demokrasia   kwani kuna baadhi  ya   Watanzania  si  wanachama  wa  vyama  vya aina  yoyote  vya  siasa  na   ameitaka  katiba  mpya  Iweke  bayana mikataba  ya Nchi  kwa  uwazi zaidi kwa  wananchi  mfano, mgogoro  uliojitokeza  MTWARA  wa  Gesi ambao umeonekana haukuwa  wazi kwa wakazi wa Mtwara  na  ardhi  iwe mali ya  wananchi   na  sio serikali  ambayo  kwa sasa hivi  meonekana  kuwepo na  migogoro  mingi hasa  pale  wanapogundua chini  ya  ardhi  kuna  madini.

Amesema vyombo vya  habari kwenye  katiba  mpya  lazima  viwe  huru  na sio  kuingiliwa  na  serikkali  hata  ikizingatiwa  kuwa  waandishi wa  habari ni kioo cha  jamii  na  si  vinginevyo, wakusanye  habari  bila  kuwepo  bugudha   na kama wanahitaji kupata taarifa  kutoka  serikalini wasinyimwe.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top