Wananchi wenye hasira kali wakibomoa nyumba ya mama Atupele Kalile akidhaniwa kuwa mchawi maeneo ya ilemi Mbeya |
Kazi ya kubomoa nyumba ya mama huyo inaendelea |
Wengine wameshaingia ndani na kuanza kutoa vyombo nje tayari kwa kuvichoma |
Mtoto wa mama Atupele akijaribu kuokoa vitu vya mama yake visichomwe moto na wanakijiji |
Vyombo vinazidi kutolewa ndani ilivichomwe moto |
Tayari wameshaanza kuchoma moto vyombo vya mama Atupele |
Mwingine anaendelea kubomoa nyumba ya mama Atupele |
Wamefyeka shamba lake lote la mahindi |
Wengine wanapongezana kwa kazi waliofanya |
Kushoto mama Atupele Kalile anaedhaniwa kuwa ni mshirikina akiwa na mtoto wake
MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Atupele
Kalile (60) mkazi wa Mtaa wa Masewe Kata ya Ilemi Jijini Mbeya amenusurika kifo
baada ya wananchi wa Mtaa huo kutaka kumpiga kisha kubomoa nyumba yake
wakimtuhumu kwa ushirikina.
Wananchi hao kumtuhumu Mwanamke huyo kuhusika na
upotevu wa motto mwenye umriwa miaka mitatu(3) (Judith Chengula) aliyepotea
katika mazingira ya kutatanisha Februai 22, Mwaka huu.
Kwa mujibu wa wakazi hao walisema Mtoto huyo
alipotea majira ya saa 11 jioni baada ya kupoteana na dada yake Anitha
Mgaya wakiwa wametokea kanisani ambapo hadi sasa mototo huyo hakuweza
kupatikana licha ya juhudi kubwa za wakazi hao kumtafuta bila Jitihada.
Walisema katika vikao kadhaa vilivyoitishwa
mtaani hapo kwa ajili ya kutafuta mbinu za kupatikana kwa mtotolakini Mwanamke
huyo hakuonesha ushirikiano jambo ambalo lilizua hofu miongoni mwa wakazi hao
hali iliyopelekea kuhisiwa kuhusika na tukio hilo.
Walisema katika kikao kilichofanyika Machi 23
Mwaka huu majira ya Asubuhi mtaani hapo wananchi hao waliendelea kusisitiza
kuwa Mwanamke huyo achukuliwe hatua kwa kuwa ndiye anayehusika na upotevu wa
motto ambapo iliamriwa kwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi.
Walisema baada ya kufika nyumbani kwake na
kufanya upekuzi walikuta vitu vinavyohisiwa kuwa vinahusika na ushirikina
ambavyo ni vitovu vya watoto wachanga watatu ambapo Mwanamke huyo baada ya
kuulizwa alishindwa kutolea ufafanuzi hali iliyosababisha wananchi kupandwa na
hasira na kuanza kumpiga.
Kutokana na tukio hilo Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa
huo Nedy Mwamlima alimnusuru Mwanamke huyo katika kipigo kutoka kwa wananchi
kwa kumpeleka katika kituo kikuu cha Polisi kwa usalama zaidi.
Baada ya mtuhumiwa huyo kunusuriwa na kukimbizwa
katika kituo cha Polisi wananchi hao hawakupoza jazba zao ambapo waliamua
kuteketeza nyumba ya mtuhumiwa ikiwa ni pamoja na kufyeka mazao yaliyokuwa
yamepandwa jirani na nyumba yake.
Hata hivyo hasira za wananchi hao hazikuishia
hapo bali walimsakama Mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la Agnes Sika
ambaye ni mke wa Mchungaji wa kanisa la Pentecost Groly kwa madai kuwa ni
rafiki wa mtuhumiwa na amekuwa akimfichia siri.
Jeshi la Polisi liliwahi kufika eneo laTukio na
kumnusuru Agnes asipatwe na madhara ikiwa ni pamoja na kutochomewa nyumba yake
ambayo tayari wananchi hao walionekana kuikimbilia kwa ajili ya kutaka
kuibomoa.
Aidha Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia
mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano zaidi pamoja na upelezi ambapo Baba mzazi wa
Mtoto anayesadikiwa kupotea katika Mazingira ya kutatanisha akisema anamwachia
Mungu baada ya juhudi za kumtafuta kushindikana.
credit: http://mbeyayetu.blogspot.com |
Post a Comment