Loading...

HABARI MBAYA KWA WANA YANGA


HARUNA Niyonzima
BONNIE MUGABE, KIGALI
HARUNA Niyonzima amemshtua Malkia wa Nyuki na kumwambia: "Nipe hayo madola mama nisaini Msimbazi."
Rahim al Kharoosi maarufu kama Malkia wa Nyuki amekuwa akifadhili mambo mengi ndani ya Simba na sasa amejitokeza kwenye harakati kuhakikisha timu hiyo inahamasika na kushinda mechi zote zilizosalia kwani wanataka nafasi mbili za juu zilizotawaliwa na Yanga na Azam.
Mwanaspoti linajua kuwa Haruna amekuwa karibu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Binkleb, ambaye muda mwingi huonekana hapa Kigali kwenye biashara zake.
Haruna maarufu kama Fabregas amewaambia matajiri wa Simba wamfuate wampe dili kwani mkataba wake umesalia miezi miwili tu na hana uhakika wa kusaini tena Yanga ingawa Binkleb amesisitiza kwamba hana presha na si Simba ya Malkia wa Nyuki au Azam ya bilionea Said Bakhresa inayoweza kumlipa asaini kwao.
Mchezaji huyo aliiambia Mwanaspoti jijini Kigali juzi Jumapili baada ya mechi ya Rwanda na Mali kuwania kufuzu Kombe la Dunia kwamba hajaamua wapi pa kwenda lakini anataka kuondoka Yanga. Mali ilishinda mabao 2-1.
Haruna alisema kipaumbele cha kwanza ni Ulaya aliko meneja wake, lakini kama hilo dili likishindikana atasaini mkataba wa muda mfupi na mmoja kati ya klabu tatu kubwa za Tanzania ambayo itakubali kukaa naye meza moja na kufika dau ambalo hakulitaja. Klabu tatu kubwa za Dar es Salaam ni Yanga, Simba na Azam.
Haruna aliyejiunga na Yanga mwaka 2010, alisema ; "Kama sitafanikisha malengo yangu ya kucheza Ulaya, nitasaini mkataba mfupi na moja kati ya klabu kubwa za Tanzania. Sijaamua moja kwa moja mpaka sasa ila mkataba wangu unaisha Mei, mwaka huu."
"Nina mipango mizuri sana ya kwenda Ulaya lakini hayo yatajulikana baada ya meneja wangu ambaye yupo Ulaya kurudi Afrika na kunipa matokeo ya klabu anazofanya nazo mazunguzo,"alisisitiza .
Alipotakiwa kuweka wazi klabu hiyo ni ipi mchezaji huyo wa zamani wa Etincelles na Rayon Sport za Rwanda alisema: "Yeyote atakayekubalia na na matakwa yangu kifedha nitamfanyia kazi ya uhakika na ataona utaalamu wangu."
"Sina uhakika kama nitasaini tena Yanga lakini kama Simba au Azam wakija vizuri tukikubaliana dau nitasaini mkataba. Nitasaini klabu yoyote kati ya hizo, lakini itategemea pia na mipango ya meneja wangu, mimi ninachoangalia ni matakwa yangu kimasilahi si jina la timu,"alisisitiza mchezaji huyo aliyejiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili kwa mshahara wa dola 1,500 (Sh 2.4 milioni) kwa mwezi.
Haruna amekuwa msaada mkubwa kwa Yanga inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya pointi 11.
Yanga ina ponti 48, Azam ya pili kwa pointi 37na Simba ya tatu na pointi zake 34.
MWANASPOTI



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top