ASKARI Polisi,Venance Kamugisha aliyejeruhiwa katika vurugu zilizosababisha vifo vya
mwananchi mmoja na Askari Polisi PC
Yohana anasafirishwa kwa ndege kupata
matibabu zaidi katika Hospitali ya
taifa Muhimbili Jijini Daressalaam .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedit Nsimeki
amewaambia waandishi wa habari kuwa majeruhi huyo alisafirishwa jana jioni kwa ndege ya abiria kwenda
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo zaidi.
Alisema kuwa hali ya Askari huyo inaendelea vizuri ambapo
juzi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu alimtembelea Askari huyo katika
Hospitali ya Mkoa huo kumjulia hali majeruhi huyo wa tukio ambalo limezua
mjadala mkubwa katika mkoa wa Ruvuma na Nchini kwa ujumla.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mko
huo Dkt Philis Nyimbi anasema kuwa wamefanikiwa kumtibu mgonjwa huyo na hali yake inaendelea vizuri na kwamba baadhi ya vipimo alivyofanyiwa uchunguzi
vimeonesha kuwa hana tatizo.
‘Lakini kutokana na majeraha ya kichwani imelazimika
apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili
katika kitengo cha mifupa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo zaidi ambavyo katika
Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma hatuna’alisema
Daktari huyo.
Alibainisha kuwa katika Hospitali hiyo hawana kipimo cha
Computer Temography(TC SCAN) ambacho kinatumika kuangalia ubongo na ndicho
ambacho Askari huyo anatakiwa akafanyiwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Jijini Daressalaam.
Machi 23 mwaka huu katika kijiji cha Ngwinde Wilayani
Namtumbo Mkoani Ruvuma Askari Polisi PC Yohana mwenye namba 7771 aliuawa na
wananchi waliochukizwa na Askari huyo
kumfyatulia risasi mwendesha Pikipiki na kumuua.
Wananchi hao walimuua
askari huyo kwa mawe na kumjeruhi PC Kamugisha ambaye alijeruhiwa baada ya
kupigwa kwa mawe wakati wakimuua Askari mwenzake PC Yohana ambaye mwili wake umesafirishwa kwenda
wilayani Kibondo Mkoani Kigoma kwa mazishi.
Post a Comment