Loading...

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limetangaza majina ya wenyeviti wapya wa kamati za kudumu za Bunge

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limetangaza majina ya wenyeviti wapya wa kamati za kudumu za Bunge, huku baadhi ya kamati zikiundwa upya na nyingine kufanyiwa mabadiliko.

Miongoni mwa kamati mpya ni pamoja na Kamati ya bajeti, itakaayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Mhe Andrew Chenge


Mkurugenzi wa shughuli za bunge John Joel amesema kutokana na unyeti wa kamati hiyo ya bajeti iliwapa mgumu katika uteuzi wa Mtu wa kuiongoza…


Na baadaye akatoa ufafanuzi Kuhusiana na kubadili utaratibu wa kujadili bunge la bajeti kuhusu vyanzo na mgawanyo wa fedha za serikali..


Mbali na kamati ya bajeti kamati zingine zinazoendelea, zilizochaguliwa upya na zilizofanyiwa mabadiliko ni pamoja na Kamati ya kudumu ya bunge ya fedha na uchumi itakayoongozwa na Mohamed Mgimwa na makamu wake Luke Kitandula, Kamati ya hesabu za serikali PAC ikiongozwa na Zitto Zuberi Kabwe na makamu Deo Filikunjomb.

Kamati ya hesabu za serikali za mitaa LAAC itakayokuwa chini ya Rajab Marouk Mohammed na Seuleiman Zedi, kamati ya huduma za jamii chini ya Magreth Sitta na makamu wake Stephen Ngonyani, kamati ya maendeleo ya jamii itakayoongozwa na Jenista Mhagama na Saidi Mtanda.

Zingine ni kamati ya Nishati na Madini itakayokuwa chini ya Victor Kilasile Mwambalasa na makamu wake Jerome Bwanausi, kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira chini ya james Lembeli na makamu wake Abdulkarim Shah pamoja na kamati ya Miundombinu itakayokuwa chini ya Peter Serukamba na makamu Juma Kapuya.

Kamati nyingine ni ile ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI chini ya Hamis Kigwangalla na makamu John Lwanji, kamati ya Masuala ya ukimwi itakayoongozwa na Lediana Mng’ong’o na Diana Chilolo, Kamati ya ulinzi na usalama chini ya Anna Margath Abdallah na makamu wake Mohammed Khatib.

Kamati zingine ni pamoja na ile ya mambo ya nje itakayokuwa chini ya Edward Lowassa na makamu wake Mussa Zungu, Kamati ya Katiba, sheria na utawala chini ya Pindi Chana na William Ngeleja, kamati ya maadili itakayokuwa chini ya Brig..Hassan Ngwilizi na John Chiligati pamoja na ile ya kilimo, Mifugo na maji itakayoongozwa na Peter Msolwa na makamu wake Said Nkumba.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top