1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na
kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa
katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.
2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya
saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali,
Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.
3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari
walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada
ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo
iliharibiwa kwa majeraha.
4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao
uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu
kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho
pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.
5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana
ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini
kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka
wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa
watafikishwa mahakamani.
Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556
Post a Comment