KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema ipo haja ya kuangalia upya sheria ya
vyama vya siasa nchini kama ina meno ya kutosha kudhibiti vyama vinavyojigeuza
kutoka vyama vya siasa kuwa vyama vinavyopanga na kuratibu uhalifu na ugaidi
nchini. “Hivi sheria ya vyama vya siasa inasemaje juu ya vyama
vinavyojigeuza kwa makusudi kutoka vyama vya siasa na kuanza kuwa vya kupanga
na kuratibu machafuko, utekaji, uhalifu na dalili za ugaidi? Kama sheria
zilizopo hazitoshelezi zitazamwe upya ili tusije iingiza nchi kwenye machafuko
kwa kisingizio cha vyama vingi”, alisema Nape. Nape alisema huku akionekana wazi kurusha makombora hayo kwa
viongozi wa Chadema, akidai baadhi ya matukio ya kihalifu ambayo yamekuwa yakitokea
nchini yamekuwa yakipangwa na kuratibiwa na viongozi wa chama hicho kutimiza
ahadi yao ya kuhakikisha nchi haitawaliki.
“Hivi watu wanaanza kutangaza hadharani kuwa watahakikisha nchi
haitawalikiu, wakaanza kugomea baadhi ya shughuli za serikali na wanapoona
hailipi sasa wanaanza kupanga, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa uhalifu,
machafuko na sasa iko dalili dalili za vitendo vya kigaidi, bado tunawaita
chama cha siasa?”, alihoji Nape. Nape alisema anashangazwa na jinsi viongozi wa Chadema
wanavyotapatapa na sakata linalokabili baadhi ya viongozi wao wa ngazi za juu
kuhusishwa na vitendo vya kigaidi, na kwamba kinachowasumbua sasa ni dhambi
ambayo anadai chama hicho kimeipanda chenyewe kwa muda mrefu. “Rafiki zangu hawa wamepanda mbegu chafu kwa muda mrefu. Wenzetu
waliamua kujenga Chama kwa msingi wa chuki na uongo, sasa walisahau mwisho wa
chuki aibu mchimba kisima huingia mwenyewe”, alisema Nape.
Nape alidai anasikitika kwa nini Chadema kimeamua kujimaliza,
kwa kijijenga katika misingi ya kujigengea umaarufu kwa kusema uongo na chuki
na mafarakano vitu ambavyo sasa vinaanza kuwaumbua kwa kuwa njia ya mwongo ni
fupi na mshahara wa dhambi ya uongo ni mauti. Alisema CCM kimeendelea kuwa Chama bora kwa sababu kilijengwa
tangu awali katika misingi ya haki na kujali wananchi na kuweka bayana misingi
yake ya uongozi. “Ndiyo sababu hadi sasa kinaendelea kutawala, lakini ni kwa
sababu ukiona vinaelea vimeundwa”, alisema Nape.
Nape alisema, baada ya CCM kufanya kazi ya ukombozi na
kuwaunganisha Watanzania na kuwa kitu kimoja, sasa kinafanyakazi ya kuboresha
maisha ya Watanzania kwa kuwa kazi hiyo ya ukombozi na kuunganisha watu
ilikwisha kamilika kwa ufasaha mkubwa. Alisema, lisema katika jitihada zake za kuwaletea wananchi
maendeleo, imehakikisha kila eneo la Tanzania linawekwa kwenye mipango ya
maendeleo ukiwemo mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro. “Hawa Chadema wanawadanganya Moshi, eti kwa kuwa wao ndiyo wenye
Halmashauri kwa hivyo wao ndiyo wameleta maendeleo. Huu ni ungo mkubwa”,
alisema, Nape nakubainisha kwamba mipango yote ya maendeleo inayotekelezwa
katika Halmashauri ya Moshi, ni utekeleza wa ilani ya CCM kwa sababu mipango
yote ipo na imeandikwa katika ilani ya chama hicho.
Akizungumzia Chadema, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Vijana Chadema (BAVICHA), Juliana Shonza aliwataka Watanzania kuacha kuwaunga
mkono Chadema katika mipango yao ya maandamano ya mara kwa mara ambayo
yanavuruga nchi.
“Vijana jihadharini sana na hawa Chadema, msipumbazike na
kugeuzwa asusa zao, maana wao huandaa maandamano ili wawapige picha kisha picha
hizo huzipeleka kwa wafadhili wao kwa ajili ya kujipatia fedha, je na ninyi
fedha hizo huwa mnapewa?”, alihoji Shonza. Akianza kuhutubia, Nape aliwaomba wananchi kusimama kwa dakika
moja kuwaombea na kuwakumbuka wale wote walioathiriwa na matendo mbalimbali
aliyodai hufanywa na Chadema, hatua iliyofuatiwa na mamia kwenye mkutano huo
kusimama kwa dakika moja na kisha kusema amina kabla ya kuketi chini.
“Kwani uongo? kwani wewe hujatambua kwamba Chadema wamekuwa
wanapanga na kuratibu matendo ya kihalifu na kigaidi, kwa kweli ni heri
tukawakumbuka na kuwaombea walioathirika na vitendo vya chama hiki”, alisema,
Juma Shangali mkazi wa Kiboriloni, Moshi. Katika mkutano huo, vijana 65, wakiongozwa na aliyekuwa Makamu
Mwenyekiti wa Chadema wa wanafunzoi wa vyuo Vikuu, Juma Ramadhani anayesoma
Chuo Kikuu cha Ardhi walirejea CCM na kuabidhi kadi zao za Chadema kwa Nape.
Source: The habari (March 2013). Nape aishutumu CHADEMA kupanga uhalifu. Retrieved from The habari
Post a Comment