WATUMISHI wa Mamala ya ya maji safi na usafi wa mazingira Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma(SOUWASA) wamepatiwa mafunzo ya kuzuia na kupambana na rushwa ili waweze kutoa huduma bila kutoa rushwa na kuifanya kazi yao ipasavyo.
Mafunzo hayo yametolewa jana kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo yakiendana na maadhimisha ya wiki ya maji Nchini ambayo huuadhimishwa kila mwaka kuanzia Machi 16 hadi 22 huku yakiendana na sughuli mbalimbali zinazohusu masuala ya maji.
Akizungumza kwenye Mafunzo hayo Afisa uchunguzi mwandamizi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) mkoani Ruvuma Bw. Hamisi Kidulani alisema kuwa rushwa ni mbaya kwa kuwa inakwamisha maendeleo na kuwaonea wanyonge.
‘Sote tuna kila sababu ya kuichukia rushwa kwa kuwa inawanyima haki maskini na kuzua migogoro katika jamii ambayo inapelekea uvunjifu wa amani’alisema Afisa huyo wa TAKUKURU ambaye alimwakilisha Kamanda wa Taasisi hiyo Mkoa wa Ruvuma.
Akiichambua rushwa ya uchaguzi alisema ni mbaya sana kwa kuwa kuna kundi la watu wenye pesa wanaweza kuwanunua Wanasiasa kwa kuwagharama gharama za uchaguzi na kuwamiliki wabunge na kisha kumnunua Rais ambapo miswada yote bungeni inakuwa inapitishwa kwa maslahi yao.
Kidulani alisema kuwa rushwa ndogo inazaa rushwa kubwa ambapo rushwa kubwa inazaa vipato duni kwa watumishi na kwamba rushwa kubwa inatokana na tamaa na kufafanua kuwa rushwa ndogo inatokana na njaa kali kwa wananchi.
Akitaja madhara ya rushwa alisema kuwa ajali nyingi barabarani zinatokana na rushwa kutokana na barabara kutengenezwa kwa kiwango cha chini baada ya Kandarasi za barabara kutolewa kwa rushwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SOUWASA,Mhandisi Francis Kapongo ameishukuru Taasisi hiyo kwa kuwapatia mafunzo hayo na kuomba yawe yanatolewa mara kwa mara ili kuwakumbusha na kubainisha kuwa mafunzo hayo yataongeza ufanisi katika kutoa huduma.
Mwisho
Post a Comment