WATU wawili wakazi wa eneo la mtaa wa mkuzo katika halmashauri ya manispaa ya songea wanashikiliwa na polisi mkoani Ruvuma kwa tuhuma za mauwaji ya fundi selemala Benjamini Mkwaya (45) ambaye awali ilidaiwa kuwa amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya nyumba yake.
Wanao shikiliwa na polisi wametajwa kuwa ni Jeruada Ndimbo (28) ambaye ni mke wa marehemu Mkwaya na John Maurusi (35) maarufu kwa Jina la Manywele ambaye ni awalayake Jeruada ambaye ni mke wa marehemu Mkwaya wote wakazi wa Mkuzo Manispaa ya Songea
Habari zilizopatikana jana mjini songea ambazo zimesibitishwa na kaim kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma zimesema kuwa tukio hilo lilitokea machi 10 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi uko katika eneo la mtaa wa mkuzo ambako taarifa za awali zilidai kuwa Mkwaya alikutwa akiwa ananing’nia kwenye dali ya nyumba yake .
Kaimu kamanda chiposi alifafanua kuwa taarifa za awali ambazo zililetwa kwenye kituo cha polisi cha songea mjini zilieleza kuwa Mkwaya alikutwa ndani ya nyumba yake akiwa amejinyonga kwa kamba ya manila na kwamba polisi walipokwenda kufanya ukaguzi kwenye eneo latukio walishindwa kubaini chanzo cha tukio hilo.
Alibainisha zaidi kuwa baadaye polisi waliendelea kufanya upelelezi wa ndani zaidi ndipo walipopata taarifa toka kwa raia wema kuwa Mkwawa aliuwawa na watu akiwemo mke wake Geruada Ndimbo (28) ambao wanadaiwa kuhusika na mauwaji ya Mkwaya ambapo alimtaja mtuhumiwa mwingine kuwa ni John Murusi (35) maarufu kwa jina la Manywele mkazi wa mtaa wa mkuzo ambaye anadaiwa kuwa ni hawala yake Jeruada ambaye ni mke wa Mkwaya.
Alieleza kuwa inadaiwa kuwa Mkwaya aliuwawa na watuhumiwa hao kisha walimfunga kamba ya manila shingoni na kumtundika kwenye moja ya boliti za dali ya chumba cha nyumba aliyokuwa anaishi na kutoa taarifa kwa afisa mtendaji wa mtaa kuwa Mkwaya amekutwa akiwa ananing’inia kwenye paa la nyumba yake.
Aliongeza kuwa baada ya mtendaji wa mtaa baada ya kupata taarifa hizo aliwasiliana na kituo cha kati cha polisi cha songea ambapo askali polisi walikwenda kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na mganga na kuikuta maiti ya mkwaya ikiw inaning’inia kwenye dali ya chumba alichokuwa anaishi na kwamba polisi mara tu baada ya kutoka kwnye eneo la tukio hilo walijipanga na kuanza kufanya upelelezi wa kina ambapo ulibainika kuwa chanzo ni wivu wa mapenzi .
Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa Mkwaya wakati wa uhai wake kwa muda mwingi alikuwa anamtuhumu mke waka Jeruada kuwa amekosa uhaminifu katika ndoa yao jambo amabalo lilipelekea kutembea na wanaume wengine akiwemo mtuhumiwa wa tukio hilo John Maurusi .
Hata hivyo kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma alisema kuwa mtuhumiwa John Maurusi maarufu kwa jina la Manywele alikamatwa juzi mchana kwenye eneo la makabuli ya Mkuzo wakati wa mazishi ya malehem Mkwaya na mke wake Jeruada alikuwa amesha kamatwa na kwamba upelelezi wa tukio hilo bado unaende lea na utakapo kamilika washitakiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauwaji.
Post a Comment