Loading...

SERIKALI INA MPANGO WA KUREJESHA SHERIA YA VIBOKO SHULENI KULINDA NIDHAMU YA WANAFUNZI

 
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema ina mpango wa kurudisha viboko mashuleni kama sehemu ya mpango mkakati wa kuboresha na kuinua kiwango cha elimu nchini.

Pia imepiga marufuku matumizi ya simu za mkononi kwa wanafunzi hao kutokana na kuchangia kuporomoka kwa elimu na maadili hali inayotishia uwepo wa taifa la mambumbu kwa miaka ijayo.
Ni katika uzinduzi wa mfumo mpya wa usomaji kwa njia ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA baina ya Walimu na Wanafunzi wa kupitia mtandao.

Naibu Waziri na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo anabainisha mipango mipya ya kurejesha nidhamu katika masomo…Naibu Waziri Mulugo anasema mfumo huo wa elimu kwa mtandao utasaidia kukabili uhaba wa vitabu na kubainisha kuwa ipo haja kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia sekta ya elimu badala ya kuelekeza lawama kwa serikali.

Faraja Nyalandu ni Mwanzilishi wa mfumo huo na hapa anaelezea jinsi wanafunzi watakavyonufaika na mfumo huo. Mfumo huo ni sehemu ya mpango mkakati wa kuboresha elimu bora nchini ikiwa ni pamoja na kwenda sambamba na ukuaji wa sayansi na teknolojia mfumo ambao umeshika kasi kwenye sekta za maendeleo ya nchi nyingi duniani.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top