Na Gideon Mwakanosya –Songea Yetu
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamsaka Mohamed Said Mkazi wa Mjimwema katika halmashauri ya manispaa ya Songea kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtoto wake wa kike ambaye anasoma darasa la sita katika shule ya msingi Samola iliyopo katika manispaa hiyo.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimezibitishwa na kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma revocatus Malimi zimesema kuwa mwanafunzi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa inadaiwa amekuwa akilawitiwa na kubakwa na baba yake mzazi tangu oktoba mwaka jana .
Malimi alifafanua kuwa inadaiwa saidi alikuwa akimtishia mtoto wake kuwa asiseme kwa mtu yeyote na kwamba taarifa hiyo ikisikika atamuua kwa kuwekewa sumu kwenye chakula au kumchinja kwa kutumia panga.
Alisema kuwa kufuatia vitisho hivyo Saidi anadaiwa kuwa alikuwa akifanya kitendo hicho cha kufanya mapenzi na binti yake mara kwa mara kwani mke wake alikuwa ameachana naye miaka mingi iliyopita.
Alifafanua zaidi kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa mtuhumiwa alikuwa ameachana na mke wake tangu mwaka 2009 na kumuachia mtoto huyo mama yake Hadija Mohamed Hitima mkazi wa Tunduru.
Alieleza zaidi kuwa mpaka oktoba mwaka jana saidi alipolazimika kumfuata mtoto wake alikokuwa anaishi Tunduru na mama yake mzazi kisha kumleta songea ili aendelee kuishi naye.
Kamanda Malimi alieleza zaidi kuwa Saidi alipofika songea mjini alianza kumueleza mtoto wake kuwa anapokwenda kulala usiku asiwe anafunga mlango wa chumba chake na baadaye alianza kuingia kwenye chumba hicho na kuanza kumrubuni na alipoona mtoto anamkataa ndipo alipoanza kumpa vitisho kisha alifanikiwa kutembea naye.
Malimi ambaye pia ni Afisa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Ruvuma alisema kuwa inadaiwa mwanzoni mwa mwezi januari mwaka huu baba mzazi wa mwanafunzi huyo aliaga anaenda shambani ambako binti huyo hakufahamu ndipo mtoto huyo alipata nafasi ya kutoa taarifa kwa majirani ya hali halisi aliyokuwa anafanyiwa ya kufanya mapenzi na kulawitiwa na baba mzazi na baadaye majirani walimsaidia kumpeleka kwenye kituo kikubwa cha polisi cha songea mjini.
Alisema kuwa taratibu za uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zimefanywa licha ya kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa msichana huyo ameingiliwa sehemu zake za siri na mzazi wake kama alivyojieleza yeye mwenyewe na polisi inaendelea kumsaka mtuhumiwa ili afikishwe mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
1 comments:
Mungu wangu huyu baba atakuwa na shida katika kichwa chake nikiwa kama mzazi naweza kusema apewe hukumu inayotakiwa kwani kamuharibia binti maisha yake kabisa.Pole sana binti na pia nakupa hongera kwa ujasiri wako wa kutoa taarifa kwa majirani.
ReplyPost a Comment