Na Nathan Mtega,Songea
Wafanyabiashara wa maduka wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamelazimika kufunga maduka yao kwa zaidi ya masaa matano kwa ajili ya kuzungumza na uongozi wa manispaa na mkuu wa wilayaya Songea kuhusiana na omgezeko la tozo a leseni kwa wafanyabiashara.
Hatua hiyo ya wafanyabiashara kufunga maduka ilifikiwa leo baada yakutokuwepo na makubaliano baina yao na uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Songea ambao ulidaiwa kukiuka makubaliano ya awali ya pamoja yaliyofikiwa baina ya uongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara,uongozi wa manispaa ya Songea na mkuu wa wilaya.
Makubaliano hayo yalikuwa ni kuangaliwa upya kwa viwango vya tozo za leseni vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria ya kodi iliyotungwa na bunge la jamhuri ya muungano ambayo haikuangalia uwezo wa kiuchumi uliopo kwa halmashauri za wilaya,miji na majiji nchini na kwa mzunguko wa fedha uliopo katika mji wa Songea wafanyabiashara waliomba pamoja na kuwepo kwa sheria hiyo wao kutazamwa kulingsana na mzunguko wa kiuchumi uliopo.
Wakati mazungmzo hayo yakiendelea baina ya viongozi na jumuiya ya wafanyabiashara wa mkoa wa Ruvuma uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Songea uliamua kuendesha msako kwenye maduka kwa ajili ya ukaguzi wa leseni msako ambao ulitumia nguvu zaidi za jeshila polisi kwa kushirikianana askari mgambo kitendo ambacho kiliwafanya wafanyabiashara waamue kufunga maduka yao kwa ajili ya kutoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na suala hilo.
Akizungumza katika mkutano huo wa wafanyabiashara mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya pamoja na kutumia muda mwingi kuwaomba radhi wafanyabiashara kwa mkanganyiko huo uliojitokeza miongoni mwao na uongozi wa halmashauri wa Manispaa huku akiwaonyeshea kidole wataalamu wa halmashauri ya ya Manispaa kwa kutoa ushauri usio sahihi kwa viongozi wao na kusababisha mkanganyiko huo.
Amesema lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa mfumo ulio sahihi na rafiki kwa kila mmoja na siyo matumizi ya mabavu kwa wafanyabiashara na ili serikali iweze kutoa huduma muhimu kwa wananchi kunapaswa kuwepo kwa mfumo sahihi wa ukusanyaji wa mapato hayo huku akilaani matumizi ya askari wa jeshi la polisi katika ukaguzi huo wa leseni.
Aidha amewashauri viongozi wa jumuiya ya wafayabiashara na uongozi wa manispaa ya Songea kuimarisha mahusiano chanya miongoni mwao ili kuweza kuijenga manispaa hiyo kiuchumi na pamoja na kushirikiana na mbunge wa jimbo la Songea mjini Leunidas Gama aweze kufikisha kilio hicho cha wafanyabiashara wa manispaa ya Songea cha ongezeko kubwa la tozo la leseni bungeni ili mapitio yaweze kufanyika.
Naye mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiasharawa mkoa wa Ruvuma Titus Mbilinyi aliwahakikishia viongozi wa halmashauri ya manispaa hiyo na mkuu wa wilaya kuwa kuwa wafanyabiashara hawapendi kufunga biashara zao kila wakati na wanatambua umuhimu wa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yao na taifa bali kinachogomba kwao ni mfumo wa ukusanyaji kodi na kauli za baadhiya watendaji wa mamlaka zilizopo.
Post a Comment