Loading...

Sungusungu wageuka kero Songea

Baada ya kutokea mauaji wa raia wengi katika mji wa songea mkuu wa mkoa na wananchi kwa ujumla walikubaliana kuanzisha ulinzi wa sungusungu ambao utasaidia katika kuimarisha ulinzi kwa kushirikiana na jeshi la polisi. Baada ya kuanzishwa kwa ulinzi huo hali imekuwa shwari kwani mauaji yametulia kama sio kwisha kabisa toka doria hiyo ya sungusungu kuanzishwa.

Cha kushangaza kama sio kustaajabisha walinzi hao wa sungusungu katika baadhi ya maeneo wamekuwa kero. Hayo yametokea katika baadhi ya maeneo ambayo taarifa zake nimezipata. Kero hizo zimetokea katika barabara iendayo Peramiho, baadhi ya watu wenye magari wamekuwa wakisimamishwa na vijana wanaoshiriki ulinzi huo huku wengi wao wakiwa wamelewa na kutishia amani kwa watu hasa wenye magari. matukio mawili ya kutishia usalama wenye magari yametokea maeneo ya Chabruma, Ofisini na Likunyu fusi. Mtoa taarifa wa kwanza amesema alisimamishwa eneo la likunyu fusi wakati anaongea na walinzi hao wengine walizunguka katika tairi za nyuma na kuanza kutoa upepo baada ya kuona hali hiyo aliondoa gari lake maana aliona hakuna usalama, wa pili alisema katika eneo hilohilo alisimamishwa na walinzi hao lakini kabla hatahamaki alihisi hali ya hatari kwa matendo waliyokuwa wanaonesha vijana hao hivyo akaamua kuto simama lakini vijana hao walikuwa wametegesha misumari katikati ya barabara hivyo kusababisha gari kupata pancha.

Kwa hali hiyo walinzi hao wamegeuka kero kwa raia. Yawezekana wapo wengi wapatao kero mbalimbali toka kwa walinzi hao. 1 comments:

This comment has been removed by the author.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top