Loading...

Ya Simba na Yanga yazikumba Majimaji na JKT Mlale

Wakati uongozi wa Simba ukitoa baraka kwa wanachama wake kuishangilia Zamalek ya Misri siku ikicheza na Yanga bofya hapa , hali hii kwa namna moja ama nyingine imezikumba timu za mkoa wa Ruvuma Majimaji na JKT Mlale, wapenzi wa soka wa hapa Ruvuma wanaonesha kutokuwa na ushirikiano katika kuzishangilia timu za mkoa huu, kitu ambacho kinadidimiza soka la mkoa wa Ruvuma.

Ushauri kwa wapenzi na mashabiki shime tuungane na kuzishangilia timu zetu, iwe Majimaji ama JKT Mlale kwani mafanikio ya timu hizo ni mafanikio ya mkoa wa Ruvuma. Tuige mfano wa wenzetu wa mkoa wa Mbeya wao wanaushirikiano ndio maana timu zao zinafanya vizuri pia watu wa Iringa wamejenga umoja kwa kuunganisha nguvu baina ya washabiki na viongozi wa timu ya Polisi na wale wa Lipuli. Ndio maana timu ngeni zikienda kucheza Iringa kupata ushindi huwa huwa ni kazi ngumu. Angalia yaliyo wapata Majimaji walipo kuwa Iringa walifungwa na kuchapwa bakora, walipofika Mbeya walipata kipigo cha magoli 6 toka kwa Mbeya City. Jamani tuache Usimba na Uyanga kwa maendeleo ya Ruvuma.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top