Loading...

Majimaji yapata kichapo nyumbani

Timu ya soka ya majimaji ya mjini hapa jana ilipata kichapo cha 2-1 toka kwa timu ya small kids. Small kids wakicheza kwa kujiamini kama wapo nyumbani ilhali wao ni wageni waliweza kuandika bao lao la kwanza katika dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza. Huku wakishangaliwa na wakazi wa songea small kids waliweza kutawala katika kipindi chote cha kwanza huku Majimaji wakipoteana.


(Mashabiki mkoa wa Ruvuma wakiishangilia timu ya Small Kids baada ya kupata bao la kwanza)

Baada ya kipindi cha pili kuanza majimaji walionesha dalili za uhai na kufanikiwa kusawazisha bao na kufanya matokeo kuwa 1-1. Wakati majimaji wakifurahia walau kupata  sare hiyo ya 1-1, kibao kiliwageukia na mnamo dakika ya 80 small kids walipata bao la pili ambalo liliwachanganya majimaji na kuwafanya waweweseke, huku mashabiki wao wakionesha kutokubaliana na goli hilo. mara baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha kumaliza mchezo mashabiki wa majimaji walimfukuza refa huyo ili wampe kichapo lakini askari polisi walifanikiwa kumuokoa mwamuzi huyo.

Wakati hayo yakitokea dereva mmoja wa gari aina suzuki alitaka kusababisha ajali ndani ya uwanja wa majimaji baada ya kuendesha gari hilo kwa mwendo kasi. Mashabiki wenye hasira walifanikiwa kulizuia gari hilo huku wengine wakilipiga mawe na kuvunja kioo cha nyumba. Katika tukio hilo polisi walifanikiwa kumtia nguvuni dereva huyo na kuwakamata baadhi ya mashabiki walio lishambulia gari hilo.


(Polisi wakimdhibiti shabiki aliyekuwa akishambulia gari)
Katika hali nyingine inayoonesha kuhatarisha afya za washabiki wa soka katika uwanja wa majimaji mwandishi wa habari hii ameona hali ya uchafu wa kukithiri katika vyoo vya uwanja huo, hali inayoonesha hakuna usafi wowote unafanyika katika vyoo hivyo. Ukiingia katika vyoo hiyo unapokelewa na harufu kali ya uchafu (kinyesi na mkojo). Rai kwa viongozi na waangalizi wa uwanja wa majimaji waangalie jinsi ya kusafisha vyoo hivyo.

(Moja ya vyoo ndani ya uwanja wa majimaji)




Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top