Loading...

Dereva aliyeua asakwa na Polisi

Na Gideon Mwakanosya, Songea
 
JESHI la polisi Mkoani Ruvuma linamsaka Dereva aliyefahamika kwa jina moja la Katwila aliyekuwa akiendesha gari lililokuwa likitoka Songea mjini kwenda Dar es salaam ambalo limedaiwa kuigonga pikipiki na kusababisha kifo cha mwendesha pikipiki hapohapo katika eneo la Bombambili Manispaa ya Songea.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amemtaja aliyekufa kuwa ni Yassin Ally (32) ambaye ni mfanyabiashara maarufu Songea Mjini na ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00  jioni huko katika eneo la Bombambili kwenye barabara itokayo Songea kuelekea Njombe.
 
Amefafanua zaidi kuwa gari hilo lenye namba za usajili T 707 AJA aina ya Scania ambalo lilikuwa lina tela lake lenye namba T 719 AHL ambalo lilikuwa likiendeshwa na Katwira ambaye alitoroka pasipojulikana mara tu baada yakutokea ajali hiyo.
 
Amesema kuwa gari hiyo inadaiwa kuwa iliigonga pikipiki yenye namba za usajili T 369 ARQ aina ya Sanlg iliyokuwa ikiendeshwa na Yassini Ally ikitoka Msamala kwenda Songea mjini na kumsababishia kifo chake hapohapo.
 
Kamuhanda amesema kuwa kwa sasa hivi polisi inaendelea kumsaka Dereva huyo na kwamba mara atakapo patikana taratibu zitaandaliwa za kumpeleka mahakamani ili kuweza kujibu mashtaka yatakayo mkabili na chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa ni mwendo kasi wa lori hilo ambalo lilimsababishia dereva kushindwa kumulimudu.
 
(Mwili wa Yassin Ally ukiwa katika gari la polisi ukipelekwa chumba cha maiti)Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top