Loading...

MKURUGENZI WA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA ATISHIWA KUUAWA

 
Na Stephano Mango, Songea

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawasaka watu wasiofahamika wanaodaiwa kumtishia kumuua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Mussa Zungiza(56) ambaye inadaiwa kuwa alitumiwa ujumbe wa maandishi kwenye simu yake ya mkononi akitishiwa kuuawa .

Akizungumza na http://www.stephanomango.blogspot.com/ jana mchana ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea machi 25 mwaka huu majira ya saa za mchana huko katika wilaya ya Namtumbo .

Kamanda Kamhanda alieleza zaidi kuwa inadaiwa mnamo siku tofauti za mwezi machi mwaka huu huko katika wilaya ya Namtumbo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Zungiza alipokea ujumbe wa maandishi kupitia kwenye simu yake ya mkononi akitishiwa kuuawa.

Alibainisha zaidi kuwa kwenye simu hiyo ya mkononi ujumbe huo ulitoka katika namba mbalimbali za simu,ambapo ujumbe wa kwanza ulitumwa machi 14 mwaka huu majira ya saa 1:46 asubuhi na ujumbe wa pili ulitumwa mach 14 mwaka huu majira ya saa 4:08 usiku .

Alieleza zaidi kuwa ujumbe huo ulieleza kuwa siku yoyote Zungiza atauawa kwa njia ya aina yoyote na kutoeleza chanzo au sababu ya kutaka kumuuwa ,jambo ambalo lilimpa hofu kubwa juu ya maisha yake .

Kamanda Kamhanda alisema kuwa Mkurugenzi Mtendaji huyo Zungiza baada ya kupokea ujumbe huo kupitia kwenye simu yake ya mkononi hatua ya kwanza alichukua ya kuwasiliana na kamati ya ulinzi ya wilaya hiyo na kisha alitoa taarifa juu ya ujumbe huo aliotumiwa wa vitisho katika kituo cha polisi cha wilaya ya Namtumbo ambako lilifunguliwa jalada la uchunguzi .

Hata hivyo kamanda Kamhanda alisema kuwa jeshi la polisi mkoani Ruvuma linaendelea na upelelezi zaidi wa kina kuhusiana na tukio hilo ili kuwabaini watu waliohusika kumwandikia ujumbe kupitia simu yake ya mkononi ambao ulimtishia kumuuwa Zungiza.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top