Loading...

ZITTO KABWE AITIMULIA VUMBI CCM KAMPENI ZA UDIWANI MANISPAA YA SONGEA


Na Stephano Mango, Songea

WANANCHI wametakiwa Kuonyesha hasira zao kwa watawala kwa kuwachagua wagombea udiwani waliosimamishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)katika Kata saba nchini ambazo zinafanya uchaguzi mdogo aprili mosi mwaka huu pamoja na ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za udiwani Kata ya Lizaboni Manispaa ya Songea Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Madizini

Kabwe alisema kuwa tunajitahidi sana kulalamika kwenye majukwaa mbalimbali lakini kama wananchi hamta onyesha hasira zenu wakati wa uchaguzi kwa kuipumzisha Ccm madarakani na kuipatia Chadema fursa ya kuongoza hii nchi haitakuwa na maana yoyote

Alisema kuwa kila mwananchi mwenye hasira ya kunyimwa mbolea ya ruzuku, kupanda kwa gharama za maisha, kukosa madawa hospitali, kukosa maji, elimu bora, kukosa miondombinu basi anapaswa kuichagua Chadema ili iweze kuwatumikia wananchi bila upendeleo

Alisema kuwa mwananchi kama kweli amechukizwa na mauaji yaliyofanyika Songea hivi karibuni na mambo mengine mengi ambayo wamekuwa wakifanyiwa wananchi na Serikali ya Chama cha Mapinduzi wanatakiwa kuipumzisha sasa Ccm madarakani

Alieleza kuwa uchaguzi huu mdogo unapaswa uwe salamu tosha kwa watawala kuwa watanzania mmechoka na utawala usiozingatia haki za binadamu hivyo hasira zenu zinapaswa zionyeshwe kwenye sanduku la kura

“ Watanzania hamna siraha kubwa itakayoweza kuwatisha watawala zaidi ya kuwakataa kwenye sanduku la kura kwani mkiandamana watawapiga risasi, mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na virungu hivyo muda wa kuionyesha siraha yenu ni sasa kwenye uchuguzi wa aprili mosi mwaka huu” alisema Kabwe

Alisema kuwa siku hiyo wananchi mnapaswa kuonyesha hasira zenu kwenye sanduku la kura hivyo tumieni vizuri fursa hiyo adimu kwa kuikataa Ccm kwani kura yenu ni zaidi ya kumpata Diwani hivyo kura yenu ni sauti yenu mnapaswa kuitimia vizuri siku hiyo

Alieleza zaidi kuwa kila sehemu utakayopita utasikia wananchi wakilalamikia matatizo ya mbolea ya ruzuku kutokana na mfumo wa ufisadi ulionea kwenye dhana hiyo unaosababisha adha kubwa kwa wananchi

Alifafanua kuwa mbolea ya ruzuku ni ufisadi mwingine unaotokana na fedha za wananchi kwani bunge lilipisha bilioni 60 kwa ajili ya kuagiza mbolea ya ruzuku ili wananchi waweze kukombolewa katika kilimo lakini wananchi hawanufaiki na ruzuku hiyo huku Serikali ya Ccm ikiendelea kunufaika na ufisadi huo

“ Ili wakala aweze kugawa mbolea anatakiwa ahonge ndipo asambaze mbolea kwa wananchi na ili wananchi waweze kunufaika nao wanalazimishwa watoe rushwa hali inayopelekea gharama za mbolea ya ruzuku kuwa kubwa kuliko bei ya mbolea ya kawaida” alieleza Kabwe

Naye Mbunge wa Vitimaalu Chadema Chiku Abwao alisema kuwa uchaguzi mdogo ni njia ya rejareja ya kuiondoa Ccm madarakani na inapofika uchaguzi mkuu ni njia ya jumla ya kuiondoa madarakani Ccm kwa kuwa haina jambo jipya la kuwaambia watanzania hivyo uchuguzi huu unapaswa kuipiga chini Ccm na kuinyong’onyesha kabisa na kwamba utakapo fika uchaguzi mkuu ni kuidondosha kabisa

Abwao alisema kuwa wananchi wa Manispaa ya Songea mmenyanyaswa vya kutosha sasa ni wakati wenu wa kusema basi kwa kumchagua diwani wa Chadema ili awe mtetezi wenu wa kweli kwa maslahi ya wananchi wote

Alisema kuwa wananchi wa Kata ya lizaboni mnapaswa muone fahari kumchagua mgombe wa Chadema Mlongo kwani ni mtu jasiri na mwenye mipango ya maendeleo katika kata hii hivyo tumia kura yako kwa kumchagua kiongozi makini na mchapa kazi wa kweli

Akizungumza kwenye mkutano huo Makamu mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Juliana Shonza alisema kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa lolote lile dunia na ndilo chimbuko la maendeleo lakini ni kundi ambalo limekuwa likipuuzwa nchini

Shonza alisema kuwa Ccm imeshindwa kutambua mchanga wa vijana katika nchi hivyo vijana wenyewe wanapaswa kuchukua hatua ya kuwakataa watawala wanaotokana na chama hicho ili waweze kupata neema katika nchi

Alisema kuwa katika uchaguzi huu vijana wanatakiwa kutuma salamu kwa watawala kwa kuipigia kura Chadema na kulinda kura hizo mpaka Diwani kupitia chama hicho aweze kutangazwa mshindi ili aweze kushirikiana na vijana katika ujenzi wa Songea na Taifa kiujumla

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime alisema kuwa wagombea wa Ccm wanapaswa wawaeleze wananchi walichofanya toka waanze kuiongoza nchi hii kwani ni miaka 50 sasa

Fuime alisema kuwa wagombea hao hawapaswi kutoa ahadi mpya kwasababu ahadi hizo walikwisha kuzitoa katika uchaguzi mkuu wa 2010 hivyo sasa wanapaswa kuwaeleza wananchi toka wakati huo wametekeleza jambo lipi

Kwa upande wake mgombea wa udiwani Kata ya Lizaboni Alanus Mlongo aliwaomba wananchi wamchague ili awe mwakilishi wao wa kweli katika kata hiyo ambayo kwa muda mrefu sasa imesimama kutokana na kutokuwa na viongozi wanaojali maslahi yao

Mlongo alisema kuwa akiwa Diwani hatakubali kuona wananchi wakiteseka kwa kudhurumiwa haki zao na viongozi wasio na dhamira ya dhati ya kusaidiana na wananchi kuleta maendeleo stahiki ili kuyafikia maisha yenye ustawi stahikiPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top