Loading...

AKUTWA AMEKUFA NA KUHISIWA KABLA HAJAFA ALIBAKWA

 MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Mary Jonathan (23) Mkazi wa Mateka katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvvuma amekutwa akiwa amekufa kandokando ya mto Ruvuma na inasadikiwa kuwa kabla ya kuuwawa alikuwa amebakwa na watu kadhaa wasiofahamika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea April 5 mwaka huu majira ya saa za asubuhi ambapo inadaiwa kuwa Mary alikutwa amekufa huku akiwa uchi wa mnyama pia alikutwa na jeraha upande wa kushoto wa kichwa chake.

Hata hivyo Kamanda Kamuhanda alisema kuwa Polisi inaendelea kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo ambalo bado linaonekana kuwa na utata kwani inadaiwa kuwa Mary aliondoka nyumbani kwa wazazi wake walioko eneo la Mateka kwenda Mahakama ya Mwanzo ya Songea Mjini ambako alikuwa amekwenda kusikiliza kesi yake ya kutishiwa kuuwawa

Kwa mujibu wa baba yake mzazi wa Mary Sajent Jonathan wa Gereza la Mahabusu Songea ni kwamba Mary alitoka nyumbani April 4 mwaka huu majira ya saa za asubuhi na aliaga kuwa anaelekea Mahakamani kusikiliza kesi aliyokuwa amemfungulia mtu mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake anayedaiwa kuwa alimtishia kumuua kwa maneno.

Sajenti Jonathan alieleza zaidi kuwa mtoto wake tangu alipoondoka April 4 mwaka huu majira ya saa za asubuhi nyumbani kwake hakurudi hadi April 5 mwaka huu majira ya saa za asubuhi alipokutwa akiwa amekufa huku akiwa na jeraha moja upande wa kushoto wa kichwa chake.

“Ninawaambia ndugu zangu kuwa mtoto wangu Mary tangu alipoondoka juzi mpaka jana asubuhi ndiyo ameonekana akiwa ameuwawa na watu wasiofahamika na sasa hivi taarifa ya tukio hilo iko Polisi nafikiri ndiko taarifa kamili mnaweza mkazipata” alisema Sajenti Jonathan.

Alisema kuwa mwili wa marehemu hivi sasa umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Serikali ya Mkoa Songea na taratibu za mazishi zinatarajiwa kufanywa mara tu Polisi watakapomaliza uchunguzi wao.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top