Loading...

ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUKUTWA NA KETE 225 ZA MADWA YA KULEVYA

Na Gideon Mwakanosya, Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Hamza Mnadi (27) mkazi wa Mtaa wa Kalanje Wilaya ya Tunduru kwa tuhuma za kukutwa akiwa amehifadhi madawa ya kulevya aina ya Cocaine na Heroine  ambayo thamani yake bado haijafahamika
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo limetokea aprili 7 mwaka huu majira ya saa 11 jioni huko katika mtaa wa Kalanje mjini Tunduru
Alieleza kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio askari Polisi wakiwa doria walipewa taarifa toka kwa raia wema kuwa kuna mtu anafanya biashara ya madawa ya kulevya katika mtaa huo na kwamba tangu alipoanza biashara hiyo kumekuwa na watu wengi wamekuwa wakifika kwenye nyumba hiyo ya Mnadi kwa lengo la kununua madawa hayo
Alifafanua kuwa Askari hao baada ya kupata taarifa toka kwa raia wema walikwenda mpaka kwenye eneo la nyumba ya Mnadi ambako walifanikiwa kumkuta na baadae walipofanya upekuzi kwenye nyumba hiyo walimkuta akiwa na madawa ya kulevya ya Cocaine na Heroine yakiwa yamehifadhiwa kwenye paketi tisa
Alieleza zaidi kuwa madawa hayo ambayo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye paketi 9 ambapo kila paketi kulikuwa kumehifadhiwa vipande 25 na kufanya jumla ya vipande 225 vya madawa hayo kwenye paketi zote 9 zilizokutwa ndani ya nyumba yake
Alisema kuwa kwa hivi sasa mtuhumiwa anashikiriwa na Polisi na upelelezi wa Polisi bado unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabilI
MWISHO
MBARONI KWA KUKUTWA NA BUNDUKI NA RISASI KINYUME CHA SHERIA
Na Gideon Mwakanosya, Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linamshikilia Lameck Ruben Halfan (38) mkazi wa eneo la Mtaa wa Aroma, Tabata Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kukutwa akiwa na siraha aina ya Riffle na risasi zake mbili kinyume na sheria za nchi
Akizungumza na Kahama Fm jana Ofisi kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 9 mwaka huu majira ya saa 2 usiku huko katika kijiji cha Angalia kilichopo Wilaya ya Tunduru
Kamanda Kamhanda alisema kuwa siku hiyo ya tukio Askari waPolisi wakiwa kwenye doria ambao walikuwa wanashirikiana na Askari wa Wanyamapori wa Wilaya hiyo walimkamata Halfan akiwa na siraha yenye namba za usajiri 083972 ambayo ilikuwa na risasi mbili ambayo alikuwa ameifunga kwenye nguo zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye begi
Alifafanua zaidi kuwa mtuhumiwa huyo Halfan alikamatwa akiwa anatokea Kijiji cha Mwenge ambako inadaiwa kuwa anajishughulisha na shughuli za uwindaji haramu wa wanyamapori akielekea mjini Tunduru
Hata hivyo Polisi bado inaendelea kufanya upelelezi zaidi wa tukio hilo na kwamba utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma mashtaka yanayomkabili



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top