Loading...

BEI YA MCHELE NA UNGA YAPANDA KWA KUTOPATIKANA UMEME KWA WAKATI‏

Na Gideon Mwakanosya, Songea
 
BEI ya unga wa mahindi na mchele katika halimashauri ya manispaa ya songea  mkoani Ruvuma imepanda  kwa zaidi ya asilimia 100 baada ya shilika la umeme Tanzania (TANESCO) kushindwa kusambaza umeme kwenye baadhi ya maeneo  ambako kunamashine ya kusaga nafaka Mjini Songea .
 
Uchunguzi ulifanywa na nipashe kwa zaidi ya mwezi mmoja umebaini kuwa bei ya unga wa mahindi ambayo hapo awali ilikuwa ni shilingi 500 kwa kilo hivi sasa kilo moja ya unga wa mahindi ni shilingi 1200 na bei ya mchele kwa miezi iliyopita kabla ya tatizo la umeme halijaanza kujitokeza kama ilivyo sasa ilikuwa ni shilingi 1000 kwa kilo lakini hivi sasa kilo moja ya mchele ni kati 1800 hadi 2000.
 
Uchunguzi umebaini zaidi kuwa bei hizo zinaendele kupanda siku hadi siku kutokana na TANESCO  kushindwa kutoa huduma ya umeme kwenye maeneo ya manzese, Mfaranyaki , Bombambili, Majengo, Lizaboni Mjimwema na Msamala ambako ndiko kuna mashine nyingi zinazo saga nafaka  na badala yake umekuwa ukiwashwa kwa mgao ambao ratiba yake haufahamiki  kwa wamiliki wa mashine hizo.
 
Mmoja wa wamiliki wa mashine za kusaga nafaka katika eneo la manzese amabye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema kuwa katika eneo hilo ndio pekee kuna mashine nyingi za kusaga nafaka mjini hapa lakini upatakani wa umeme ni mgumu sana ambapo baadhi ya wafanya biashara wamekuwa wakileta mpunga kwa ajili ya kukoboa lakini imekuwa ikishindikana kutokana na kutopatikana umeme na badala yake wafanya biashara hao wamekuwa wakichukua mpunga huo kukoboa makambako kukoboa kisha mshele kuurudisha songea kuuza kwa bei kubwa .
 
Ameliomba shirika la umeme  Tnzania (TANESCO) kuona umuhimu mkubwa wa kupeleka umeme kwenye maeneo  ambayo yanamashie za kusaga nafaka ili kupunguza gharama za uendeshaji kwa wafanya biashara wa mazao hasa ikizingatiwa kuwa mpunga umekuwa ukinunuliwa maeneo ya Lusewa wilayani Namtumbo na Muhukulu wilayani Songea Vijijini na kuletwa songea mjini kwa ajili ya kukoboa lakini yamekuwa yakikubwa na adha kubwa la umeme la kulazimika kusafirisha tena kwenda Makambako mkoani Ruvuma kwa ajili ya kukoboa .
 
Kwa upande wake Ofisa masiko wa manispa  ya songea Salum Omela alizisibitisha kuwa bei ya unga na mchele katika masoko mbalimbali mjini hapa imekuwa ni kubwa kwa zaidi ya asilimia 100 ambapo amatoa mfano kuwa bei mchele imekuwa ikiuzwa kati 1800 hadi 2000 kwa kilo wakati awali imekuwa ikiuzwa shilingi 100 na baei ya unga apo awali ilikuwa shilingi 500 wakati hivisasa ni shilingi 1200 kwakilo .
 
Meja wa Halmashauri ya manispaa ya songea Charles Muhagama alisema kuwa baraza la manidiwani limeridhia hali halisi ya upatikanaji wa umeme kwani hivi karibuni walipata nafasi ya kutembelea kwenye kituo caha Kibrag;oma kinamashine ya kufulia umeme na walikuta mashine ya kufulia ummeme aliyoileta Raisi Jakaya Kikwete ikiwa inaendelea kutoa umeme na kwamba kwa hivi sasa TANESCO iko kwenye jitihada kubwa kumaliza tatizo hilo ambalo limeonekana ni tatizo kubwa kwa wakazi wa songea  
 
Meneja wa TANESCO mkoa wa Ruvuma  Mwandisi  Monica Kebala  alisema kuwa tatizo la kuto patikana umeme wa mara kwa mara muda wote kwa hivi sasa limepungua licha ya kua bado umeme unatolewa kwa mgao kwa sababu  ufuaji umeme umepungua kutokana na kuharibika kwa baadhi ya mitambo ambapo kwa hivi sasa mashine tatu kati ya mashine saba zilizopo ndio zinazo saidia kutoa huduma ya umeme mjini Songea.
 
Alisema mashine tatu zinazofanya zinazalisha umeme megawaiti 2.6 wakati mahitaji kwa wakazi wa manispaa ya songea ni megawati 5 hasa ikizingatiwa kuwa  songea kuna wateja 12,000 hivyo bado umeme utaendea kutolewa umeme kwa mgao lakini maeneo muhimu kama hospitali, ofisi za serikali na kambi za jeshi umeme utaendelea kutoleawa.
 



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top