Loading...

MBARONI KWA TUHUMA ZA KUCHOMA MOTO NYUMBA NNE TOFAUTI‏

Na Gideon Mwakanosya, Songea

 
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Zakalia Kapinga ambaye umri wake haukuweza kufahamika mara moja mkazi wa kijiji cha longa kilichopo wilayani Mbinga kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba nne zilizo ezekwa kwa nyasi katika matukio matatu tofauti na kusababisha kuungua mali mbalimbali  zenye thamani ya shilingi 745,000.
 
Akizungumza na KAHAMA FM jana ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma  mrakibu mwandamizi wa polisi  (SSP) George Chiposi alisema kuwa matukio hayo matatu yalitokea juzi majira ya saa za usiku kwa nyakati tofauti huko katika kijiji cha Longa wilayani Mbinga .
 
Alisema kuwa inadaiwa mnamo may 11 mwaka huu kwa nyakati tofauti Kapinga alichoma moto nyumba nne ambazo zilikuwa zinamilikiwa na wakazi watatu wa kijiji cha longa ambapo aliwataja kuwa ni Theobati komba, Welnet Ndunguru na Sabasi Haule .
 
Alifafanua zaidi kuwa siku hiyo ya tukio majira  ya saa 6: 30 usiku huko katika kijiji cha longa Komba na familia yake wakiwa wamelala Ghafla walishituka kuona nyumba zao mbili  zinateketea kwa moto na waliptoka nje ya nyumba hiyo walimwona Kapinga akiwa anakimbia kisha walipiga kelele kwa ishala ya kupata msaada zaidi kutok a kwa majirani na baadaye Komba alipofanya tasimini baaaday ya kuungua nyumba na mali zake aligundua kuwa mali zake zenye thamani ya 350,000 zimeteketea kwa moto.
 
Alibainisha zaidi kuwa muda mfupi tu baada ya kutokea  tukio la kwanza ghafla Ndunguru akiwa amelala nyumbani kwake na familia yake alishituka baada ya kugundua nyumba yake kuchomwa na moto ambapo majirani walifika kwenye eneo la tukio na kufanikisha kuwaokoa watoto wa liokuwa wamelala ndani ya nyumba hiyo lakini mali yenye thamani ya 290,000 iliungua kwa kuteketea na moto
 
Alieleza zaidi kuwa wananchi wakiwa wanaendelea kuzima moto nyumba ya ndunguru katika hali ambayo ilikuwa si ya kawaida nyumba nyingine ya Haule nayo ilianza kuungua moto na kusababisha mali yenye thamani ya 105000 kutekete kwa moto   ambapo kutokana na jitihada za majirani familia yote ya Haule iliokolewa licha ya kuwa vitu mbalimbali yakiwemo mahindi na maharage viliteketea kwa moto .
 
Hata hivyo kutokana na juhudi kubwa ya wananchi wa kijiji cha longa mtuhumiwa wa matukio yote matatu Kapinga alikamatwa usiku uleule mara tu matukio hayo kutokea na alipelekwa kwenye kituo kikuu cha polisi wilayani mbinga ambako anaendelea kuhojiwa zaidi
 
 
Kahimu kamanda SSP Chiposi alisema kuwa kufuatia kutokea matukio yote matatu ya nyumba nne zilizoezekwa kwa nyasi kuungua na moto hakuna madhara ya aina yeyote yaliyotokea  kwa familia hizo zilizo kumbwa na matukio hayo ya nyumba zilizo teketea kwa moto na polisi imemshikilia mtuhumiwa Kapinga na inaendelea kufanya uchunguzi wa kina zaidi ili kubainini chanzo cha matukio hayo na utakapo kamilika atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayo makabili.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top