Loading...

Kumewaka Songea: Leo CHADEMA kufanya maandamano kupinga mgao wa umeme.

Leo kuanzia muda wa saa 5 asubuhi, chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) mkoa wa Ruvuma kitafanya maandamano ya amani yatakayoanzia kuanzia Mfaranyaki, wakipitia barabara ya Mbinga/Sokoine road na kuzunguka hadi maeneo ya benk ya NBC na NMB na pale kituo kikuu cha polisi na kumalizia soko la samaki. Dhamira ya maandamano hayo ni kushinikiza serikali kutoa tamko la ufumbuzi juu ya mgao wa umeme unaoendelea kwa takribani miaka minne mfululizo. Katibu wa CHADEMA jimbo la Songea bwana Masumbuko Geoge jana alikuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani hapa. Tatizo la umeme mjini Songea limekuwa sugu kwani umeme unaweza kuuona nyumbani kwa saa 2-3 kati ya masaa 24. SOURCE: Radio one NIPASHE
Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top