Loading...

MAGAZETI YAUZWA KWA BEI KUBWA SONGEA‏

Na Gideon Mwakanosya, Songea
 
UONGOZI wa Halimashauri ya Manispaa ya songea Mkoani Ruvuma umewaonya mawakala wa magazeti mbalimbali yanayoletwa Mkoani humo kuacha mara maoja tabia ya kuuza magazeti kwa bei kubwa tofauti na bei  halisi iliyoandikwa kwenye magazeti .
 
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kwani aba ya mgurugezi wa Manispaa hiyo Nachoa Zakalia Afisa biashara wa Manispaa hiyo Kelvin Charle alisema kuwa kutokana na hali iliyojitokeza kwa wauza magazeti ya kuuza magazeti kwa ulanguzi  wananchi wengi wakiwemo wasomaji wameilalamikia tabia hiyo ya kuwalangua wanaponunua magazeti hayo.
 
Alisema kuwa baada ya Manispaa hiyo kupokea malalamiko mengi  imelazimika kuchukua hatua za haraka za kuwaonya mawakala wanaosambaza magazeti mjini Songea kuwa tabia hiyo ni mbaya na inaonyesha wazi kuwa wasomaji hawaridhiki na tabia hiyo.
 
Charle alieleza zaidi kuwa amewaagiza mawakala wote wa magazeti mjini songea kuhakikisha kuwa magazeti yao yanauzwa kwa bei harali iliyopangwa na makampuni yanayochapisha magazeti hayo na si vinginevyo na kwamba mawakala watakayo kiuka agizo hilo watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuwasalianana uongozi wa makampuni ya magazeti hayo husika.
 
“Ndugu waandishi ni jambo la kusikitisha sana kwa baadhi wa mawakala wanaosambaza magazeti kuona yakiuzwa kwa bei kubwa mfano gazeti la NIPASHE AU MWANANCHI ya kiwa yameandikwa habari mzuri za uteuzi wa baraza la mawazili, wakuu wa mikoa na hivi karibuni uteuzi wa wakuu wa wilaya yamekuwa yakiuzwa kati ya 2000 mpaka 2500 badala ya bei shiling 800 iliyoandikwa kwenye magazeti na bei ya gazeti la majira ni shilingi 500 na wao walikuwa wakiuza 1000 mpaka 1500  charle alisema “
 
Hata hivyo Afisa biashara huyo alifafanua zaidi kuwa endapo hali hiyo ya ulanguzi  wa magazet ikiendelea ofisi yake italazimika kuwasiliana moja kwa moja na makampuni  yanayoleta magazeti mkoani Ruvuma ili kuangalia njia mbadara ya kukomesha hali hiyo.
 
Kwa upande wake wakala wa magazeti ya Kampuni ya The Guardian Mkoani Ruvuma Ahmedi Musa Maarufu kwa jina la Bushoke alipoulizwa na gazeti hili kuusiana na malalamiko haya alikili kuwepo  wimbi la ulanguzi wa magazeti ambapo alidai kuwa hali hiyo ilianza kujitokeza wakati magazeti yalipoaanza kuandika habari za kifo cha aliyekuwa msanii Steven Kanumba  .
 
Alisema kuwa wasomaji walianza kulalamika magazeti yalikuwa yakiuzwa kwa bei ya shililngi 2000 mpaka 2500 badala ya  bei halisi ya shilingi 800 kwa magazeti ya NIPASHE jambo ambalo amedai kuwa limemlazimu kuwa kwa karibu sasa na wauzaji wa magazeti hayo na ameomba uwepo ushirikiano wa karibu kwa wasomaji hata ikiwezekana kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama .
 
Naye muuzaji wa magazeti ya BUSSINES TAMES  wa Mjini songea Peter  Mlelwa alisema kuwa baadhi ya wauzaji wa magazeti wamekuwa wakikiuka tarabu wanazo pewa na mawakala wao amabao wamekuwa wakiwaonya kuacha uuza magaeti kwa bei kubwa na badara yake wauza magazeti hayo wamekuwa wakikaidi kuuza magazeti mfano lgazeti la Majira likiwa linahabari ya Kanumba, baraza la mawaziri au hivi karibuni uteuzi wa wakuu wa wilaya limekuwa likiuzwa shilingi 1000 hadi 1500 jambo ambalo limeonekana kuwa ni kelo kubwa kwa wasomaji .



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top