Loading...

SUGU AWAONDOA HOFU WAFANYAKAZI NA WAFANYABIASHARA ENDAPO CHADEMA ITACHUKUA NCHI

Na Gideon Mwakanosya,Songea
CHAMA cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)kimewatoa hofu  wafanyakazi wa Serikali na wafanyabiashara hapa nchini wanaokipenda Chama hicho kutokuwa na wasiwasi na nafasi zao pindi kitakaposhika dola mwaka 2015 kwa kuwa kitafanya mabadiliko kwa nafasi za juu tu na kwa upande wa wasiokuwa waadilifu.

Hayo yalibainishwa na  Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara ya habari,utamaduni na michezo,Joseph Mbilinyi wakati akizungumza na wandishi wa habari baada ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara  kwenye Viwanja vya Maroli Majengo mjini Songea.

Alifanya Mkutano huo jana wakati akihitimisha Ziara ya siku nne Mkoani Ruvuma ambapo alizoa wanachama 57 sehemu mbalimbali za mkoa huo baadhi yao wakiwa Makatibu,Wenyeviti  wa Kata na mabalozi wa CCM.

Aliwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi na  nafasi zao kwa kuwa kitakaposhika dola  kitawatumia na kufanya mabadiliko katika nafasi za juu na kuongoza Nchi kwa uadilifu na umakini wa hali ya juu.

‘Watu wamekuwa na wasiwasi na hatma ya maisha yao pindi tutakaposhika hatamu za uongozi wa Nchi,lakini nawambieni watu tutakaofanyanao kazi ni hawahawa lakini wawe waadilifu ila tutafanya mabaliko katika ngazi za juu’alisema na kuongeza

Ndugu zangu tumedhamiria kushika dola na hivi sasa tunapiga jaramba na nawaambieni Mbunge mmoja wa CHADEMA sawa na Wabunge 50 hadi 60 wa CCM na hapa tumeonyesha tuna uwezo si mnatuona bungeni tunavyojenga hoja.

Alisema Chama hicho kitakaposhika uongozi wa Nchi Wananchi watarajie usimamizi madhubuti wa  fedha za Serikali na rasilimali za Nchi kwa maslahi ya Nchi yao tofauti na ilivyo sasa ambapo fedha zinaibwa na Mawaziri wasiokuwa waaminifu na kwamba wafanyakazi hawatafukuzwa kazi.

Alisema katika ziara yake amebaini Chama hicho kinapendwa hadi vijijini na Ushahidi mkubwa ni katika kijiji cha Amani Makolo ambako ni nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM,Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Mbunge wa Songea Mkijini Marehemu Dkt. Laurence  Gama ambako wana mwenyekiti wa kijiji.

Mbunge huoyo alisema hivi sasa Chama hicho hakina mipaka na kimejitanua vijjini ambako CCM ilikuwa ikikutegemea na kwamba huko mabalozi kuna wengi walikubali kujiunga na kuwa Mbalozi wa Chama hicho.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati kuu wa Chama hicho,Mbogoro alisema kuwa kuna Mawaziri wazuri ndani ya Chama hicho ambao wanashindwa kufanya kazi vizuri kwa kukwazwa na mfumo mbovu ndani ya Serikali ya Chama cha mapinduzi.

‘Msingi wetu mkubwa utakuwa Taifa kwanza  katika kuongoza Nchi na  tutawateua watu wazuri toka Vyama vingine vya upinzani,usishangae kuona Lipumba anakuwa Waziri wa fedha CHADEMA itaposhika madaraka.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top