Loading...

Mbunge wa CHADEMA avamiwa mkutanoni watu wakatwa mapanga.

Chanzo: makambakokwetu.blogspot.com
Jana Mch. Msigwa(CHADEMA) alivamiwa katika mkutano wa chama chake uliofanyika Nduli ambapo fujo kubwa zilitokea na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa vibaya. Taarifa za awali zinasema kwamba vijana walioanzisha fujo hizo ni watoto wa diwani wa CCM wa eneo hilo ambao walifika mkutanoni kwa lengo la kumvamia Mch. Msigwa jambo ambalo lilisababisha mapigano baina yao na wafuasi wa CHADEMA na hivyo vurugu hizo kupelekea watu kadhaa kujeruhiwa. Taarifa kamili juu ya fujo hizo zitatolewa na Mch. Msigwa mwenyewe kwenye vyombo vya habari.
Mch. Msigwa akihutubia kabla ya vurugu

Wananchi wa Nduli wakimsikiliza Mch. Msigwa kwa umakini
Wananchi wa Nduli wakichukua fomu za CHADEMA kujiunga na chama hicho( wananchi zaidi ya 100 walijiunga na chama)

Mch. Msigwa akimtambulisha aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wa eneo hilo ambaye sasa kahamia CHADEMA

Kijana wa CHADEMA aliyejeruhiwa vibaya usoni katika vurugu kwenye mkutano

Kijana wa CHADEMA aliyekatwa na panga mkononi kwenye fujo.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top