Loading...

VIONGOZI WATAKIWA KUWA WAKWELI KATIKA MAJUKUMU YAO

Na Steven Augustino,Tunduru

IMEBANISHWA kuwa tabia za uongo miongoni mwa jamii yetu ndiyo chanzo cha kukosekana kwa ukweli na utendaji mbovu wa viongozi na watendaji wa Serikali na kumesababisha hali mbaya ya upatikana wa huduma za Utawala na Uchumi.

Hayo yameainishwa na baadhi ya wakazi wa Jimbo la Tunduru Kusini Wilayani humo Mkoani Ruvuma wakati wakazi hao waliposhiriki  mdahalo uliojadili Utawala Bora na uwajibikaji wa Viongozi wa serikali kwa wananchi uliofanyika katika Ukumbi wa Klasta mjini hapa.

Kufuatia hali hiyo wananchi hao pia wamedai kuwa ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji kwa watumishi serikali inapaswa kuunda mfumo utakaowawajibisha haraka viongozi wabovu badala ya kutumia muda mrefu wa kuendesha kesi

Wakizungumza kwenye mdaharo huo Selemani Kachonjo kutoka kijiji cha Lukumbule, Athuman Milanzi na Casiana Magogwa ambao ni miongoni mwa makundi ya Jamii yaliyokutanishwa na Mtandao wa Asasi za Kirai wilayani Tunduru (MATU) chini ya mwavuli wa The foundation for Civil Society, kilio chao kwa niaba ya wananchi wenzao ni kwamba watawala bado hawajawaangalia kwa jicho la Umakini wananchi wanaowatawala hususani waishio pembezoni mwa Nchini ikiwemo Wilaya yao.

Pamoja na mambo hayo wananchi hao wamelalamikia kero za kutotatuliwa kwa matatizo ya wakulima, kushamiri kwa rushwa na kile walichokiita kuwa chanzo chake ni uongo uliotawala katika shughuli zote za utoaji huduma za utawala kwa wananchi yaliyobainishwa na
Monica Mbogolo na Abdalah Mgwila.

Aidha katika ya maoni hayo pia Abdalah Kawanga na Issa Mtua kwa niaba ya wananchi wakaibua tatizo linalo wakabili wakulima wa zao la Korosho ambapo wananchi wanadai kuwa ukosefu wa uwajibikaji kwa watendaji wa serikali ndio uliosababisha mpaka leo wakose malipo yao ya pili ya Korosho walizo uza msimu uliopita.

Awali Mchokonozi wa mada katika mdahalo huo, Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani Ruvuma (TAKUKURU) Hamis Kidulani na Mwenyekiti wa Mtandao wa asasi za Kiraia Wilayani Tunduru  John Nginga walisema kuwa ili kuyafikia maendeleo ya kuanza kufaidi maziwa na asali bila ubaguzi watanzania wanapaswa kujenga utamaduni wa kuzingatia sheria.

Akifungua mdaharo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Tunduru  Afisa tawala wa Wilaya hiyo Maltin Mulwafu katika hutuba yake alisisitiza uwazi na uwajibikaji kwa viongozi na Wananchi wake na kuwataka wasikubali kuona misingi ya utawala bora inakiukwa.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top