Loading...

KATIBU WA UVCCM WA WILAYA SONGEA APANDISHWA KIZIMBANI KWA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA

Na Gideon Mwakanosya, songea

KATIBU wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) wa Wilaya ya songea a Anton Nkantala Mkoa wa Ruvuma amepanda kizimbani katika mahakama ya akimu mkazi mfawidhi  mkoani humo kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na kufanikisha kunyang’anya pikipiki .

Upande wa mashitaka ulioongozwa na wakili wa serikali kanda ya Songea Shaban Mwegole mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa ruvuma Frenk Mahimbali  ulidai kuwa Nkantala ambaye ni kiongozi mwandamizi wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) wa wilaya ya songea ameshitakiwa kuwa mnamo juni 11 mwaka huu majira ya saa za usiku huko katika eneo la mtaa wa pacha nne uliopo kata ya lizaboni manispaa ya songea aliiba pikipiki yenye namba za usajili T482 BZS aina ya SANLG ambayo nia mali ya Maxmilia Haule

Mwaigole alieleza zaidi kuwa Nkantala anadaiwa kufanikisha unyang’anyi huo kwa kumkaba shingoni mwendesha pikipiki hiyo aliyefahamika kwa jina la Savior Mapunda kwa kumzidi nguvu kisha kufanikiwa kumnyang’anya pikipiki huku akiwa anamtishia kumkata na panga na pikipiki hiyo alikimbia nayo na kusiko julikana.

Hata hivyo mwendesha mashitaka ambaye ni wakili wa serikali mwaigole aliiomba mahakama hiyo kuona umuhimu wa kutompatia dhamana mshitakiwa Nkantala kwa kuwa upelezi wa kesi hiyo bado unaendelea.

Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Mahimbali alikubaliana na ombi la upande wa mashitaka na kudai kuwa kwa kuwa upelelezi unaendelea mshitakiwa anarudishwa lumande hadi Agosti 7 mwaka huu kesi hiyo itakapo tajwa tena hasa ikizingatiwa kuwa shitaka linalomkabili Nkantala ni la unyang’anyi wa kutumia silaha ambalo ni miongoni wa shitaka halina dhamana.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top