Loading...

WAGONJWA WALIOLAZWA HOSPITALI YA SERIKALI YA MKOA WALALAMIKIA TATIZO LA UHABA WA MAJI

BAADHI  ya  Wagonjwa  waliolazwa katika  hospitali ya Serikali  ya Mkoa  wa Ruvuma wamelalamikia adha  kubwa  ya  uhaba  wa maji  kwenye  maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo  ambapo  wamedai  kuwa  wamekuwa  wakilazimika  kuyatafuta  maji  ya  kuoga  au  ya kufulia  nje  ya  hospitali hiyo kwa  gharama kubwa.

Wakizungumza  na  NIPASHE  kwa   nyakati  tofauti  jana  majira  ya saa za asubuhi  kwenye  Wodi  namba  5 na  namba  6 ambazo ni kwa ajili ya kulaza wagonjwa  wanawake  baadhi  ya wagonjwa wamesema  kuwa   kuna  uhaba mkubwa  wa  maji na  kwamba  hakuna hatua zozote  ambazo zinaonekana  kufanywa  kutatua  tatizo  hilo ambao limeonekana  nia  kelo kubwa.

Wagonjwa  hao ambao  wameomba  majina  yao  yahifadhiwe walisema  kuwa  tangu  walipolazwa  hospitalini  hapo  wamekuwa  wakipata  shida  kubwa namna  ya kupata  maji hasa wanapohitaji  maji kwa  ajili  ya  kuoga  au  kufulia  nguo  jambo  ambalo  linawalazimu watu wanaowauguza  kutoka  nje  ya eneo la hospitali  hiyo  kwenda  kuyatafuta  maji yanakouzwa  kati  ya  shilingi  500 hadi   700  kwa  ndoo  moja.

Wagonjwa  hao wameiomba  serikali   ichukuwe  hatua  za  haraka   kumaliza  tatizo  la uhaba  wa  maji linalohikumba  hospitali  hiyo na  kwamb  Uongozi   wa  hospitali hiyo ni vyema  ukaona  umuhimu  wa  kutafuta  maji hata  kwa  kuwauzia  wagonjwa  waliolazwa  hospitalini humo  kulio adha  wanayoipata  hivi sasa.

Wamsema  kuwa  tatizo  la kutopatikana   kabisa  maji  kwenye  hospitali hiyo imekuwa  ni kero  kubwa  hasa pale  wagonjwa wanapohitaji   kuoga au  kufua  nguo lakini  ni  vyema  wangewaruhusu wafanya biashara  wanaouza maji kuingia  kwenye  mawodi  kuuza  maji kwa wale  watakao  hitaji  maji.

Kwa  upande  wake  Mganga  mfawidhi  wa hospitali  ya serikali  ya Mkoa wa  Ruvuma  Dr. Benedict  Ngaiza  alipohojiwa na  NIPASHE  jana mchana  ofisini kwake  kuhusiana  na hospitali yake  kukabiliwa  na  uhaba  mkubwa  wa maji  alikili  kuwepo kwa tatizo  la  maji  ambapo  alieleza  kuwa  tatizo  hilo katika  hospitali  yake  si kubwa sana  kama  wagonjwa  wanavyolalamika.

Dr. Ngaiza  alieleza  kuwa  kumekuwepo  na  upungufu  wa  maji  katika  baadhi  ya  maeneo  ya  hospitali  hiyo  mfano:  katika  kitengo cha  maabara  ambako ndiko kuna  shida  kubwa sana  na  kukosekana  kwa maji katika  kitengo  hicho  huduma  kwa  wagonjwa  hulazimika  kusimama  kwa  muda  wakati  jitihada  zikiwa  zinafanywa  namna  ya kuyapata  maji.

Alisema kuwa   kutokana  na  tatizo  la  uhaba  wa maji uongozi wa hospitali  hiyo  umelazimika  kuchimba  kisima   cha  kuvuta  maji  ardhini  ambacho kimekuwa  kikisaidia  kwa kiasi  kikubwa  kutoa  maji  ambayo yamekuwa  yakipelekwa  kwa  baadhi  ya  maeneo  ambayo ni muhimu  hospiatalini hapo  mfano. Kwenye  maabara  na  kwenye  chumba  cha upasuaji.

Naye  mkurugenzi  wa  maji safi na maji taka  Songea  (SOUWASA) muhandisi  Frances  Kapongo alipohojiwa na  NIPASHE  jana  ofisini kwake  kuhusiana  na tatizo la  uhaba  wa maji  alisema kuwa   katika  maeneo mengi ya halmashauri  ya Manispaa  ya  Songea  kumekuwa  na uhaba wa maji ikiwa ni pamoja na  eneo  la hospitali  ya Mkoa   kwa  sababu  vyanzo vyote  vya  maji vilivyopo  katiaka  maeneo  ya  Luhila  na  kwenye  milima  ya  matogoro  vimekauka  kabisa na kwamba  tatizo hilo litakwisha   hadi  muvua  zitakapoanza kunyesha  na  si  vinginevyo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top