MWALIMU Mkuu wa shule ya msingi Nakawale iliyopo kata ya Muhukuru katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Amini Mbaraka (55) amefariki dunia papohapo baada ya kudondoka kwenye Trekta dogo (pawatila) ambalo alikuwa amepanda akielekea Songea Mjini.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa kumi jion huko katika kijiji hicho ambako mwalimu mkuu huyo mbaraka alikutwa na mauti wakati akisafiri.
Alifafanua zaidi kuwa Dereva wa pawatila hilo Ali Makalani (51) mkazi wa kijiji cha Nakawale ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi anadaiwa kuwa alishindwa kuhumudu uskani baada ya trekta hilo kufeli breki kisha ilianza kuyumba na kusababisha mmoja kati ya abilia waliokuwa wamepanda kwenye pawatila ambapo alirushwa na kumsababishia kifo chake papo hapo.
Alibainisha zaidi kuwa abilia wengine walikuwa wamepanda kwenye pawatila hilo ambao idadi yake haikuweza kupatikana mara moja na kwamba mpaka sasa haina taarifa zaidi ya majeruhi hao ambao inaonyesha wazi kuwa hali zao zinaendelea vizuri.
Kamanda Nsimeki alisema kuwa trekta dogo hilo ambalo halikuwa na namba za usajili licha ya kuwa alitaja namba za injini ya pawatila hilo kuwa ni 20911210041 ambalo lilikuwa linaendeshwa na Makalani
Hata hivyo Kamanda Nsimeki aliwaonya wananchi kuacha tabia ya kutumia usafiri wa matrekta madogo (pawatila) na badala yake kwa kuhofia maisha yao ni vyema wawe wanatumia usafiri unao eleweka na si vinginevyo.
Aidha kamanda huyo Nsimeki alisema kuwa jeshi la polisi Mkoani humo linaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo na kwamba utakapo kamilika dereva wa pawatila hilo atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
Post a Comment