Loading...

ABAKWA HADI KUFA MJINI SONGEAJESHI LA POLISI mkoani Ruvuma linawasaka watu wanaodaiwa kumbaka mwanamke ambaye jina lake limehifadhiwa mkazi wa mtaa wa mkuzo katika halmashauri ya manispaa ya Songea na kumsababishia kifo.
Habari zilizopatikana leo mjini Songea ambazo zimethibitishwa na afisa mtendaji wa mtaa wa mkuzo manispaa ya Songea bwana Shaweji Salehe zilieza kuwa mtu mmoja wa jinsi ya kike ambaye anasadikiwa kuwa na umri wa miaka(32) amekutwa akiwa akiwa ameuwawa na watu wasiojulikana.
Alisema kuwa baada ya taarifa hiyo kufika kwenye ofisi yake ndipo alipo toa taarifa ya tukio kwenye kituo kikuu cha polisi cha mjini Songea ambako alikutana na afisa upelelezi wa makosa ya jinai wa wilaya ya Songea Inspeta Anna Tembo ambaye alianza kuifanyia kazi muda mfupi tu baada ya kumjulisha juu ya tukio hilo.
Kwa upande wake kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Msimeki alipohojiwa  leo majira ya mchana ofisini kwake alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa limetokea novemba 17 mwaka huu majira ya saa za usiku huko katika eneo la mtaa wa mkuzo Songea mjini.
Msimeki alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo baada ya kutokea tukio hilo majira ya saa 12 asubuhi afisa upelelezi wa makosa ya jinai wa wilaya ya songea alipokea taarifa kutoka kwa afisa mtendaji wa mtaa wa mkuzo zilizoelezea kuwa kuna mwanamke ameuwawa na watu wasiofahamika.
Hata hivyo alifafanua kuwa uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa na mikwaruzo sehemu za shingoni, pia ilikutwa mipira miwili ya kiume (kondomu) ambayo ilikuwa imekwisha tumika iliyokuwa imeingizwa sehemu za siri za marehemu huyo na michirizi ya damu ilionekana sehemu zake za siri kitu ambacho kiliashiria kuwa mwanamke huyo alikuwa amebakwa na kunyongwa shingo baada ya kumfanyia kitendo cha kinyama.
Kamanda Msimeki alisema kuwa uchunguzi zaidi umebaini kuwa mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa miaka miwili iliyopita alikuwa ameolewa na Stambuli Njohopa na baadaye inadaiwa kuwa walitengana na miezi sita iliyopita mwanamke huyo anadaiwa kuwa alikuwa anamahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine jambo ambalo linahofiwa kuwa ndicho chanzo cha mauaji hayo.
Kamanda Msimeki alieleza kuwa kufuatia kutokea kwa tukio hilo jeshi la polisi mkoani humo wakati linaendelea kufanya uchunguzi zaidi linawasaka watu wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo ya kinyama na kwamba endapo watakamatwa watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top