Katika hatua isiyokuwa ya kawaida, hali ndani ya bunge jana jioni ilichafuka, baada ya mwenyekiti wa bunge, kushishwa kabisa kuongoza kikao hicho kufuatia kuzuka kwa malumbano makali baada ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya kukituhumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa vinara wa mgomo wa madaktari.
Manyanya alisema kuwa, CHADEMA wamebainika kuchochea mgogoro huo, hali iliyomfanya Mbunge wa Ubungo kusimama na kuomba mwongozo akimtaka Manyanya kuthibitisha ama kukanusha tuhuma hizo.
Lakini katika hali ya kushangaza, Mbunge wa Iramba mashariki Mwigulu Mchemba alisimama na kunukuu hotuba ya kambi ya upinzani, ambayo ilitamka bayana kuwa inaunga mkono madai ya watumishi wa serikali, na kwamba kwa kauli hiyo inadhihirisha bayana kuwa ndio wakuu wa mgomo huo.
Badala ya kutoa mwongozo, Mabumba hakumtaka Manyanya kukanusha ama kuthibitisha alimruhusu Mchemba kuendelea kurusha makombora mazito dhidi ya CHADEMA, safari hii akidai kuwa ni vimbelembele kutoa matamshi ya kulaani kupigwa kwa Ulimboka huku, wakimwacha mmoja wa viongozi wake bila kumhudumia wala kumjulia hali.
Katika kujichanganya kwa wabunge hao wa CCM, wakati Mchemba akidai kuwa CHADEMA ndio wachocheaji wakubwa wa mgogoro huo kwa kuwatumia madaktari, mwenzake Manyanya alitoa hoja safari hii akidai kuwa, ndio waliohusika na tukio la kumvamia na kumteka na kisha kumpiga Dk. Ulimboka.
Hata pale Mnyika aliposimama na kuomba tena mwongozo wa mwenyekiti, huku akiweka bayana jinsi inavyoelezwa ushiriki wa maafisa wa polisi, na hata Dk. Ulimboka mwenyewe kuwataja wengine kwa majina, alimtaka mchangiaji kuthibitisha ushiriki wa CHADEMA kumjeruhi ama siyo afute kauli yake.
Lakini kwa mara nyingine tena, Mabumba hakumtaka Manyanya wala Mchemba kuthibitisha kauli ama kufuta kama inavyofanywa kwa wabunge wa upinzani, badala yake alimruhusu mkuu huyo wa mkoa wa Iringa kuendelea na mchango wake bila kufuta kauli wala kuithibitisha.
Kushindwa huko kwa waziwazi kwa Mwwenyekiti wa kikao hicho cha bunge, kuliwachefua wabunge wengi wa upinzani, huku wale wa CCM wakionekana kufurahia jambo hilo.
chanzo Tanzania Daima
Post a Comment