Loading...

TAARIFA YA JUMUIYA YA MADAKTARI

KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA
02.07.2012
PRESS RELEASE

TAARIFA YA JUMUIYA YA MADAKTARI KUHUSU MAAMUZI YA SERIKALI KUFUATIA HOTUBA  YA RAIS WA  JAMHURI  YAWA TANZANIA TAREHE 1 JULAI 2012 JUU YA MGOGORO KATI YA SERIKALI NA MADAKTARI

Utangulizi

Jumuiya ya madaktari imepokea kwa masikitiko hotuba ya Serikali kuipitia Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzaina

Ifahamike kuwa mgogoro huu umedumu kwa takribani miezi saba bila kupatikana kwa suluhu ya dhati baina ya pande mbili.

Kutokana na Hotuba iliyotolewa na Mhe Rais ya tarehe 01.07.2012 kwa wananchi wa Tanzania kupitia vyombo vya habari, Kamati ya Jumuiya ya Madaktari inapenda  kutoa  ufafanuzi  katika mambo yafuatayo;

Ni wazi ikafahamika kuwa mjadala juu ya hoja /madai ya Madaktari kwa mara kadhaa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umekuwa ukizuiwa na Mhe,Spika wa Bunge kwa kigezo kuwa suala hilo liko mahakamani ,je ni sahihi Serikali kutoa maamuzi juu ya suala hilo?

Pia, kuhusu suala la kutekwa ,kupigwa na kuumizwa kikatili kwa Dr.Ulimboka Stephen,Serikali kupitia Jeshi la polisi lilitangaza kuwa Tume imeundwa ili kuchunguza suala hilompaka sasa hakuna mwenye uwezo wa kuthibitisha kuwa Serikali haijahusika moja kwa moja, je  ni sahihi kwa Mhe,Rais kutamka waziwazi  kuwa Serikalihaihusiki kwa namna yeyote ile hata kabla ya tume kutoa ripoti yake ya uchunguzi? Hii itatoa uhuru kwa tume ambayo kimsingi imeundwa na Serikali?

Nini dhamira ya Madaktari katika kusuluhisha Mgogoro huu

Kwa kuamini kuwa Madaktari ni upande muhimu katika kufikia suluhu ya dhati, tulishiriki katika meza ya ya Majadiliano kwa takribani miezi mitatu,na jumla ya vikao sita vilifanyika,katika vikao hivyo takribani vikao vine kati ya vikao sita (asilimia 66% ya vikao na muda wa vikao) tulijadiliana juu ya Uboreshaji wa huduma ya afya kwa Watanzania,ni masikitiko yetu kuwa Ripoti ya Ufafanuzi juu ya Hoja/Madai ya Madaktari ya tar 31 Juni  2012, Taarifa ya Mhe,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii ,Taarifaya Waziri Mkuu ndani ya Bunge na hata hotuba ya Rais haikuzungumzia  chochote ni kwa jinsi gani serikali itaboresha huduma za afya kwa Watanzania.

Pia tulijadiliana kuhusu Uboereshaji wa Mazingira ya Kazi,ambapo tuliishauri Serikali kupitia kamati ya Majadiliano kuwa ni muhimu kurejesha motisha kwa watumishi wa sekta ya afya kwa kurudisha posho mbalimbali ambazo ziliondolewa.

Kuhusu suala la mshahara, tulishauri serikali iwe wazi kuhusu uwezo wake wa kulipa mishahara, cha kushangaza ni kwamba Serikali imekuwa ikitoa taarifa tofauti juuya ongezeko hilo mfano,Mhe,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii amelihutubia Bunge kuwa ongezekoni 15% ,Hotuba ya Mhe,Rais metoa ongezeko la 20%. Ripoti yaWataalamu iliyotokana na Kamati ya Waziri Mkuu ilitoa pendekezo la 25%. Je nia ya Serikali iko wapi? Wakati viongozi wa Serikali wakitoa taarifa zinazotofautiana ,Ripoti ya Ufafanuzi wa madai/hoja ya Madaktari iliyotoka na Majadiliano sisi tukiwa wajumbe haikutoa pendekezo(ofa) yoyote juu ya ongezeko la mshahara.

HITIMISHO

Kwa kuwa kuendelea kufanya kazi katika mazingira haya ndugu zetu Watanzania wazalendo wengi wamepoteza maisha kutokana na ukosefu wa vifaa tiba na madawa.

Na kwa kuwa tumefanya kwai kwa miaka mingi sana tukishuhudia  haya tunadhani muda umefika wa kubadilisha hali hii na kuwasaidia ndugu zetu Watanzania.

Na kwa kuwa Serikali imeshindwa kuweka mazingira ya kazi kuwa bora na kuwezesha huduma bora kwa wananchi na watoa huduma.

Hivyo basi Madaktari Bingwa tumeamua kuacha kufanya kazi ambayo haiendani na kiapo cha Madaktari mpaka hapo Serikali itakapokubali kurejesha interns wote na kufungua meza ya Majadiliano yenye ni9a ya dhati ya kumaliza mgogoro.

 Na Wawakilishi
 Kamati ya Jumuiya ya Madaktari
 Imesainiwa na
 Katibu Jumuiya ya Madaktari.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top