Loading...

RC RUVUMA AWAONYA WALIMU WANAOENDELEA KUGOMA

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ameonya walimu wa shule za msingi sekondari na vyuo mkoani hapa kusitisha mara moja mgomo na badala yake warudi kuendelea kufundisha  hasa ikizingatiwa kuwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanajiandaa kuanza kufanya mithiani yao hivi karibuni.
Wito huo ameutoa jana wakati aakizungumza na walimu wakuu wa shule zote za halmashauri ya Manispaa ya songea  kwenye ukumbi wa chuo kikuu huria mjini Songea,amesema kila mwalimu anapaswa kutambua umuhimu alionao katika jamii hivyo ni vema kuachana na vishawishi vya kuendeleza migomo ambao unatolewa na chama cha walimu.
Mwambungu ameongeza kuwa,kwanzia sasa mwalimu yoyote ambaye hataonekana kuhamasisha mgomo kwa walimu wenzake atachukuliwa hatua kali za kisheria  kwani mgomo huo  siyo halali na tayari serikali imeshapeleka swala hilo mahakamani kwa ajili ya usuluhishi.
Amefafanua zaidi kuwa kila mwalimu kwanzia sasa hahakikishe kuwa anakuwepo katika eneo lake la kazi na anaingia darasani kufundisha na sio kwenda kusaini na kutoka kwani watakuwa wanapita na kuandika majina ya walimu ambao wamehudhuria kazini na kufundisha.
“Naomba muwaambie walimu wote warudi shuleni kufundisha kwani kila kila mtu aliomba kazi peke yake ,na ambao watakahidi agizo hili watachukuliwa hatua za kisheria,na hatuta mvumilia kiongozi yoyote ambaye ataonekana amehamasisha mgomo huo,”alisema Mwambungu.
Aidha,amewashauri walimu hao kuwa wavumilivu wakati serikali inashugulikia madai yao , nao wawape haki ya msingi wanafunzi  hao.
Kwa upande wake  katibu wa chama cha walimu mkoa wa Ruvuma Luya Ngonyani amesema mgomo huo ni halali na upo palepale kwani umezingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini hivyo  hali halisi ya mgomo mkoani Ruvuma umeitikiwa kwa shule nyingi za msingi, sekondari na chuo cha ualimu cha Songea.
Ngonyani ameongeza zaidi kuwa ni walimu wachache ambao wameonyesha kutokukubaliana na mgomo huo  lakini bado wanaendelea ili kuwashawishi waungane na walimu wenzao ili kuhakikisha kuwa mgomo huo unakwenda kama CWT ilivyotaka.
Wakati huohuo baadhi ya shule za msingi zikiwemo Matalawe, mfaranyaki, maji maji na misufini zimewarudisha wanafunzi majumbani na kuwataka kurejea shuleni hapo siku ya ijumaa ambayo shule zote zitafungwa rasmi.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top