Loading...

NCHIMBI ATOA MSAADA WA GARI LA WAGONJWA SONGEA

MBUNGE wa Jimbo la Songea mjini ,ambaye pia ni waziri wa mambo ya ndani Dkt.Emmanuel Nchimbi ametoa msaada wa gari lakubebea Wagonjwa lenye thamani ya zaidi ya shilingi 45 kwa ajili ya kusaidia wananchi wakiwemo wakina mama wajawazito.
Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Songea mjini jana kwenye ukumbi wa Songea club , Dkt Nchimbi alisema kuwa gari hilo ni sehemu ya ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za kugombea ubunge wa jimbo hilo mwaka 2010 kwenye kata ya Lizabon.
Amesema, amejipanga kuhakikisha wananchi wa Songea wanapata huduma bora zaidi na amewataka wanachama hao kuhakikisha wanaendelea kuhamasisha zaidi shughuli mbali mbali za maendeleo ili kuweza kurudisha heshima ya chama cha mapinduzi.
Dkt. Nchimbi meseikitishwa na kitendo cha baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakileta visingizio visivyokuwa na sababu za msingi kuwa wanatishiwa kuuwawa ili waweze kujipatia umaarufu.
Amesema, niabu kwa mtu mzima kusingizia kuwa ametishiwa kuuwawa ili aweze kurudi katika chati za juu, kwani tayari wananchi wameshawashitukia na wamewadharau kutokana na uzushi wao hivyo amewataka wananchi kuendelea kufanya shuguli za maendeleo na kuwapuuza zaidi.
“Kuna wakati watu walikata tamaa kutokana na chama kuonekana kuyumba lakini sasa, hali imerejea kama kawaida na chama kimezidi kuwa na umaarufu zaidi ,kutokana na wanachama wetu kuwa na imani nacho kama awali,”alisema NchimbiPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top