Huku watanzania wakipinga hatua ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kumfikisha mahakamani mtuhumiwa mmoja pekee Kati ya askari zaidi ya 6 waliokuwa wakimpiga Marehemu Daudi Mwangosi kabla ya kuuwawa kwa bomu,zipo taarifa zilizovujishwa na askari mkoani Iringa kuwa imeandaliwa mbinu chafu ya kumtetea mtuhumiwa huyo ili kuonkana kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na tatizo la mtindio wa ubongo.
Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umedokezwa na mmoja Kati ya makachero wa polisi ambao wanapinga unyama huo wa mwanahabari Daudi MWANGOSI kuuwawa kwa bomu.
Imedaiwa kuwa lengo la kutaka kufanya hivyo ni kutaka kulilinda jeshi zima la polisi na waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dkt Emmanuel NCHIMBI huku wengi wao wakihoji sababu ya Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa chini ya mwenyekiti wake mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma kuendelea kuwa Kimya hadi sasa.
Pamoja na kuhoji ukimya wa serikali ya mkoa wa Iringa pia ukimya wa Waziri mkuu na Rais Jakaya kikwete bila Kutoa rambi rambi Kama alivyozoeleka katika misiba mbali mbali ukiwemo wa msanii Kanumba na mingine huku Mauwaji haya Makubwa ambayo yameigusa tasni nzima ya habari hakuna aliyezungumzo chote chote.
via francisgodwin.blogspot.com
Loading...
Home » Unlabelled » JESHI LA POLISI LADAIWA KUPANGA MBINU CHAFU ZA KUMLINDA MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI
Post a Comment