Loading...

HUKUMU YA KESI YA GODBLESS LEMA LEO DSM

Live Feeds: Kutoka mahakama Kuu ya Rufaa Kivukoni - Rufaa ya Lema, Dec 04, 2012

Watu sio wengi sana na ulinzi haupo kabisa, ndani ya mahakama kwa sasa hatuzidi watu ishirini, Namuona Jembe Lissu na mawakili wengine, Lema bado hajafika. Kesi bado haijaanza!Updates:

Naaam Jemadari wa vita vya ukombozi Mh Lema na Aminata mmoja ya kamanda maalumu aliyejiandaa kwenda kumpumzisha Steven Ngonyani kule Korogwe ndio wanaingia ndani ya mahakama,

Watu pipoooooooo, Poweeeeerrrrrr!

Watu wanazidi kuongezeka,

Lakini ukumbi ni mdogo sana unaokadiliwa kubeba watu hamsini tu walioketi,

More Updates:

Watu wanazidi kuongezeka, lakini jambo lakufurahisha kama si kusikitisha nikuwa upande wa walalamikaji (ccm) hawapo hata mmoja yani ndani ya mahakama ni mwendo wa kombati za ukombozi tu,

Kwaupande wa Mr Lema anaonekana ni mwenye furaha na nilipojaribu kuongea nae anajiamini sana, hili linaleta matumaini kwa safari ya ukoombozi dhidi ya mkoloni mweusi!

Kesi bado haijaanza, lakini kwaujumla nikuwa watu wote wamejaa tabasamu la kudumu!

Nashukuru kuona makamanda vijana maarufu ndani ya chadema na hapa jf kama Kileo na Sanane wapo ndani ya mahakama!

More Updates:

Naaam kwa amri ya mtukufu askari wa mahakama, anatuamru tuzime simu, ila mimi nitajitahidi kukaidi kwa manufaa ya wana jf!

Bado kesi haijaanza, tunamsubiri jaji

More Updates:

Naaaam Jaji ameingia sasa ni ailiiiiiiiiii kooooooti!

Sasa tulieni mbwembwe tuache!

Mida ya kesi ya kesi hii

More Updates:

Watu wamegoma kusikiliza kwa kiingereza, sasa ni mwendo wa kiswahili tu!

Wakili wa upande wa jamhuri anaomba muongozo wa baadhi ya kanuni za usikilizaji,

Jaji anatoa ufafanuzi kwakusema wataanza kusikilizwa upande wa warufani

Wakili wa Lema ndugu Kimogoro anaanza kuzisoma hoja za upande wa wakata rufaa (lema) na ufafanuzi kwa uchache!

More Updates:

Wakili wa Lema mr Kimomogoro anaendelea kutoa mifano ya kesi za kufanana na hii ya Lema zilizoamriwa na mahakama hii ya rufaa, ambapo anaiomba mahakama hii iamue kama zilivyoamriwa hizo!

Jaji anaonyesha kustuka kidoogo hasa baada ya kutoa mfano wa kesi ya zamani ya Kiwanga, jaji anahoji kuwa nikweli iliamuliwa na mahakama hii?

Wakili anajibu ndio, anamwelekeza mahali ilipo, jaji anakubali na sasa wakili anaendelea kufafanua!

More Updates:

Wakili wa Lema anaendelea kusoma hoja za mrufani na mifano ya kesi za kufanana nayo,

Watu sasa ni wengi wamejaa na kusimama!

More Updates:

Jaji anahoji kuwa waliofungua kesi ni kweli hawakuwa wahusika?

Wakili anajibu ndio ni kweli,

Jaji anahoji je unaitaka mahakama hii iamini kuwa hawakuwa wahusika?

Wakili anajibu ndio,

Jaji anahoji kuna ushahidi unaoweza kuiaminisha mahakama hii?

Wakili anajibu basi anakubaliiana na huo muongozo kwakuwa hawakuwa na ushahidi wakutosha,

Hoja ya nne sasa inaendelea!

More Updates:

Hali ya utulivu imechukua nafasi yake, watu wanasikiliza kwa makini hoja za kisheria,

Karani wa mahakama anamwambia wakili aongeze spidi ya kusoma hoja!

More Updates:

Katika hoja ya kumi, wakili anahoji ilikuwaje ushahidi wa walalamikaji uliodaiwa kuwa ni wa CD haukuonyeshwa mahakamani lakini miaka 10 tu nyuma katika kesi ya Warid Kaburu uliletwa ushahidi wa cd na ukatolewa mahakamani live?

Wakili anazdi kuhoji Jaji wa mahakama kuu kule Arusha alirdhikaje na ushahidi huo?

More Updates:

Mapaka sasa tupo hoja ya kumi na tano,

Mtazamo wangu mpaka sasa kwa hoja hizi, ninaona ushindi wa haki na wawazi wa Mh Lema, labda yale ya magogoni yajitokeze!

Hoja zinandelea kutolewa....

More Updates:

Wakili amemaliza kusoma hoja zote 18,

Anaiomba mahakama hii kutengua hukumu ya mahakama kuu kanda ya Arusha,

Anataka upande wa (ccm) walipe gharama zote za uendeshaji wa kesi hii toka mahakama kuu mpaka hapa ilipo fikia!

Wakili wa jamuhuri anazungumza sasa, kabla hajaendelea anatulizwa chini na jaji isha wakili wa pili wa Lema anaendelea kutoa ufafanuzi wa taratibu za uchaguzi nchini.


More Updates:

Wakili wa pili wa Lema, anasema kisheria mpiga kura hana haki ya kwenda mahakamani kufungua kesi kwa kosa lililotokea wakati wa KAMPENI za uchaguzi,

Anafafanua kuwa katika uchaguzi wowote wahusika huwa watatu,
1)Mgombea
2)Mpiga kura
3)Msimamizi wa uchaguzii

Kila mtu anamipaka yake ya kuhusika,

Anazidi kusema, sheria inamtaka yeyote ambae anaona haki YAKE imekiukwa anayo haki ya kwenda mahakamani.

Sasa hoja ya msingi iliyomvua ubunge Lema inasema kuwa Lema alimtukana Dr Burian wakati wa kampeni.

Wakili anasema kisheria anaepaswa kufungua kesi ni Dr Burian (mgombea) na sio mpiga kura mwngine kwakuwa tukio lilitokea katika ulingo wa wagombea (kampeni)

Hoja hii inafanya ukumbi ulipuke kwa vbicheko vya furaha hasa baada ya wakili kuonyesha kujiamini na kutiririka kwa hoja murua!

More Updates:

Wakili wa pili wa Lema anasema kuwa kisheria mtu pekee anaeweza KUINGILIA na kufungua kesi ya uchaguzi ya hao watu watatu ni mwanasheria mkuu tu na sio vingine!

More Updates:

Wakili wa pili wa Lema anamalza kwakusema "Ninaunga mkono rufuni"

Jaji anaomba ufafanuzi wa kipengele cha ambacho bunge liliruhusu matusi kwa wagombea na niaina gani ya matusi,

Wakili kwa kujiamini zaidi anafafanua zaidi uukumbi unazidi kuchangamka!

Wakili wa ccm hoi ameomba dakika kumi na tano akapitie hoja zoote kisha tutarejea!


More Updates:

Naaaam mahakama imerejea,

Wakili wa ccm Alute Mgwai anaendelea kujibu hoja za mawakili wa Lema!

More Updates:

Wakili wa ccm Mgwai anasema anasikitika kuona mawakili wa Lema wamedanganya kuwa wale waliofungua kesi hawakuwa wapiga kura na hawakuwa na kadi ya mpiga kura,

Anasema kuwa walileta kadi zao za kura na zikarekodiwa namba zao lakini (hasemi kama nakala zipo au laa)

Anazidi kusema kuwa kwa wakili msomi hutakiwi kuidanganya na mahakama, na kwakusisitza zaidi ananyanyua juu kitabu cha kanuni za uwakili.

Anaendelea...

More Updates:

Hoja alizojibu wakili Mugwai mpaka sasa ni 1,2,3, 5, 6 na anaendelea kujibu

Jaji anamwambia kuwa anakiuka utaratibu wa mahakama kwa kuanza kutumia lugha ya kiingeraza wakati kesi ni maalumu kwa Kiswahili

Wakili anaomba radhi na kuendelea kwa kiswahili

More Updates:

Wakili anakili kuwa ni kweli hakukuwa na ushahidi wa mojakwamoja uliotolewa mbele ya mahakama kule arusha kuwa Lema alitukana,

Jaji anambana anasema unajua tafsiri ya mahakama juu ya kifungu hicho?

Wakili anababaika, anazidi kusema hiyo hiyo hiyo, watu wanaangua kicheko!

Quote By Ben Saanane View Post
Wakili Alute Muigwai anadai hoja ya common law haistahili kutumia Kwa kuwa tayari kuna sheria husika katika jambo lenyewe hasa sheria ya uchaguzi na katiba.

Amerejea kesi ya Dr.Slaa ya Mwaka 1997. Pia anakiri kwamba hoja ya burden of proof Ina uzito lakini Haina Athari.

Anaulizwa swali na Jaji juu ya tafsiri kwamba Kama anajua maana ya neno SATISFACTION.anapata kigugumizi. Watu wanacheka Kwa nguvu. Anapaniki analeta reference ya tafsiri Katika kesi ya Eliufoo vs Mbowe.

Kesi ya Defamation/kashfa Amerejea kesi ya Msabaha vs Kabuye na kudai ilikua msingi wa hukumu ile.
More Updates:

Wakili Mgwai anaendelea kumalizia kujibu hoja ya mwisho mawakili wa Lema.

Mtazamo wangu ni kuwa majibu yake ni mepesi kulinga na hoja husika,

Wakili anaomba ulinzi kwa jaji kwamba nyuma yake watu wanamsonya,

Haahaa jaji anamwambie endelea tu, yeye anazidi kusema mbona mawakili wenzake wa Lema walisikilizwa vizuri tu?

Sasa anaendelea...

More Updates:

Wakili wa ccm Mgwai anasema kuwa hukumu ya mahakama kuu ilikuwa halisi na ya haki,

Hivyo anaiomba mahakama hii ya rufaa isiitengue

Wakili wa ccm anasema upande wa mrufani haujaleta vielelezo au kuonyesha jinsi mashahi walivyokuwa credibility

Wakili mgwai anazidi kusema, kama upande wa lema uliamini kuwa CD ndio ushahidi wa mwisho, kwanini hawakudai pale mahakamani?

Wakili Arbati anainuka na kujibu kuwa haikuwa kazi yao kuleta ushahidi, bali wao ndio walitaka ccm wauonyeshe huo ushahidi wa CD,

Wakili Albert anakaa na Wakili Mgwai anaendelea ujibu,

Jaji anamuhoji je ni nani alitakiwa kuuleta huo ushahidi wa cd?

Wakili Mgwai anasema mwanasheria mkuu hakuona umuhimu,

Jaji anazidi kumbana kuwa hizo cd zipo wapi?

Wakili anazidi kubabaika anasema "wanazo waooo"

Jaji anasema kama unasema cd wanazo wao (lema) waombe sasa hivi na kama wakikataa mahakama itaangalia itakavyoamua,

Hali ni nzito kwa upande wa wakili wa ccm

Mara anasema hizo document (cd) wanazo (ccm) mara wanazo mawakili wa Lema,

Anasema wao hawakuwa na shida nazo ndiomaana hawakuzihitaji

More Updates:

Wakili bado anaendelea kujibu hoja japokuwa alionyesha kumaliza,

Anazidi kukazia kipengele cha maadili ya Uchaguzi, hasa kwenye matusi na ubaguzi wa kijinsia

Hoja hii inaonyesha ndio hoja ngumu katika kesi hii ingawa itahitahiji kuungwa mkoni kwa ushahidi zaidi.

Japokuwa wakili huyu Mgwai anaonyesha kuzidiwa na ugumu wa hoja, lakini ndani yake anahoja ambazo zinatakiwa kujibiwa kisheria na kikatiba.

Anamaliza kwakusema:

Anaomba gharama za mawakili wa wili zilizotumika ktk kesi hii tangu kule mahakama kuu.

Anakili kuwa rufaa hii imekuwa ngumu, imewafanya kujiandaa, kusoma na kutafuta zaidi ushahidi.

Anasema ndiomaana mpaka sasa ni saa saba amesimama,

Anasema ndiomaana hata wakili wa Lema bwana Kimomogoro ameamua kuongeza nguvu ya Lisu na Albert.

Jaji anamuuliza kuwa mlileta mashtaka makamani mkisema Lema ametukana, lakini hamjasema matusi hayo yaliathiri vipi uchaguzi huo?

Wakili anajibu kwakutumia mifano ya kesi zlizoamuliwa na mahakama hii,

Anasema suala haliaangaliii matusi yaliathiri vipi uchaguzi, bali tunasimama automatic kuwa matusi hayatakiwi.

Jaji anamuuliza, wewe ulikuwa wakili kule arusha, ulipowahoji mashahidi wako walisema matusi yaliathiri vip uchaguzi?

Wakili Mgwai anasema wale waliofungua kesi ni sehemu ya walioathirika.

Jaji anamuuliza tena je walipiga kura?

Wakili anajibu NDIO,

Jaji anamuuliza tena NIATHARI gani zilijitokeza katika uchaguzi kwa sababu ya MATUSI?

Wakili anasema hiyo ya kujua kuwa waliathrika kwa kiasi gani ni sheria ya Uingereza, lakini sisi Tanzania tunasimamia sheria za uchaguzi na matusi ni mwiko,

Jaji anamwambia akae.

Wakili wa Lema bwana Tundu Lissu anaanza kujibu hoja za wakili Mgwai

Anaanza kujibu hoja ya cd,

Anasema ushahidi wa video na cd ulikuwa ni wa ccm na sio wa chadema,

Anazidi kusema kuwa katika barua za walalamika amabo zipo kwenye kumbukumbu za kesi hii walisema wazi kuwa wanaoushahi wa video na cd,

Lakini jambo la katika jambo la kushangaza hawakuvleta mbele ya mahakama kama ushahidi, zaidi walisema walipeleka kwa msimamizi huo,

Lisu anazidi kusema kama kweli walikuwa na ushahidi huo, kwanini hawakuuleta mahakani? Waliogopa nini?

Anaendelee kujibu hojo za Mgwai na kusema anawasiwasi na elimu yake.

Quote By Ben Saanane View Post
Tundu Lissu Anaendelea kusema mahakama ijiulize ni Kwa nini Jaji aliyetoa hukumu hakuangalia standard of proof hata Kwa lip service na kupelekea uamuzi usiolingana na muongozo wa sheria.

Hakuzingatia hata hoja zilizotokana na na mawakili katika kesi zilizopita.

Anadai Pia kifungu namba 88 kime-elaborate kuhusu mambo ambayo ni offence Kwa mujibu aw sheria za uchaguzi.Anadai illegal practices ni makosa ya jinai.

Anakiri reference ya kesi ya Kiwanga iliamuliwa na sheria ya ya uchaguzi Mwaka 1970,Kama ambavyo sasa mahakama haijawahi tangu Mwaka 1980 kusema kwamba kuna sheria mpya.

Wakili Muigwai ameinamisha kichwa.

Naona wana-CCM wanaondoka m4c waliopo nje sasa wanachukua nafasi zilizoachwa wazi
Quote By Ben Saanane View Post
Lissu anadai kama kulikuwa na matusi basi kanuni na sheria ya maadili ilitakiwa itazamwe na ni Adhabu gani ilistahili.

Anasema petitioners ambao Si wagombea,tume ya uchaguzi Hawana haki sawa katika kupanga Matokeo ya uchaguzi.

Anadai mgombea haki yake ni ya kuchaguliwa Kwa hiyo Anasema kifungua kesi ya kudai Kwamba amedhalilishwa kwa matusi na haki yake ya kuteuliwa au kuchaguliwa imekuwa violated.

So the right petitioner here is Batilda Salva Buriani
Updates:

Mh Lema akizungumza nje ya Mahakama, amesema anashukuru mungu kwakuanza kusikilizwa kwa kesi hii,

Amesema, nanukuu "Mimi nilichaguliwa na wanachi wa Arusha, zaidi ya kuchaguliwa kwa kura, lakkini wananchi wa Arusha Mungu aliwapa kiongozi wao ambae ni mimi, na mungu atawarudishia kiongozi wao ambae ni mimi"

Akaenda mbali zaidi kwakusema, bado anaamini kuwa IKULU iliingilia kesi hii, hivyo hata kama atashindwa kesi hii, atamshangilia Mungu kwani Mungu anamakusudi nae!


CHANZO: JF

Quote By Ben Saanane View Post
Kesi imeahirishwa hadi Kesho
Attached Thumbnails Attached Thumbnails
Click image for larger version. 

Name: mahakamani-leo.jpg 
Views: 0 
Size: 134.9 KB 
ID: 73587Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top