Loading...

MWANAFUNZI ABAKWA HADI KUPOTEZA FAHAMU MKOANI RUVUMAJESHI LA POLISI mkoa wa Ruvuma limefanikiwa kumtia mbaroni Daud Ndunguru (19) wa mtaa wa Hoahoa uliopo Mbinga mjini na linaendelea kumsaka na mwingine jina lake ambaye halikufahamika mara moja linaendelea kumsaka kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kike wa umri wa miaka 12 (jina lake limehifadhiwa) anayesoma darasa la nne katika moja ya shule za msingi zilizopo Mbinga mjini na kumsababishia maumivu makali na kupoteza fahamu.

Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Msimeki zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea desemba 2 mwaka huu huko katika mtaa wa Kihaha nje kidogo ya Mbinga mjini ambako mwanafunzi wa kike inadaiwa alibakwa na watu wawili akiwemo Daud Ndunguru ambaye alikamatwa muda mfupi baada ya kumfanyia kitendo cha kinyama msichana huyo  na mwenzake ambaye jina lake halikuweza kufahamika alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Habari zaidi za tukio hilo zimefafanua zaidi kuwa watu hao wawili akiwemo Ndunguru majira ya saa 4:30 usiku walimvizia njiani msichana huyo na kumlazimisha atoe nguo alizokuwa amevaa na kisha kumfanyia kitendo cha ubakaji jambo ambalo limesababisha msichana huyo kupata maumivu makali sehemu za siri na kusababisha kupoteza fahamu.

Hata hivyo kamanda Msimeki alisema kuwa kufuatia kuwepo kw purukushani hizo majirani watoka na kwenda kwenye eneo la tukio ambako walifanikiwa kumkamata Ndunguru na mwenzake alikimbia huku msichana huyo akiwa amepoteza fahamu na walimchukua na kwenda nae kituo cha polisi cha kati cha polisi ambapo walichukua hati ya polisi ya matibabu (PF3) na kwenda nae hospitali ya serikali ya wilaya ya Mbinga ambako amelazwa na anaendelea kupata matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Kamanda Msimeki alisema kuwa mtuhumiwa Ndunguru anatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi upelelezi wa tukio hilo utakapo kamilika na jeshi la polishi mkoani Ruvuma linaendelea kumsaka mtuhumiwa mwingine wa tukio hilo anayedaiwa kukimbia na kutokomea kusikojulikana baada ya kumfanyia kitendo cha kinyama msichana huyo


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top