Loading...

askari auwa kwa wivu wa mapenzi songea

JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamsaka Payi milinga (28) mkazi wa kijiji cha masangu kilichopo magagula wilaya ya Songea kwa tuhuma za kumjeruhi kichwani kwa kutumia chupa ya soda iliyovunjika na kumsababishia kifo askari mwanafunzi wa jeshi la kujenga taifa (JKT) kambi la Mlale.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma mrakibu mwandamizi wa polisi George Chiposi alisema kuwa tukio hil9o limetokea januari 14 mwaka huu majira ya saa za jioni huko katika kijiji cha masangu ambako Peter Haule (21) ambaye ni askari mwanafunzi wa jeshi la kujenga taifa inadaiwa kuwa aliuwawa na Milinga kwa kuchomwa na chupa ya soda iliyokuwa imevunjwa na mtuhumiwa huyo.

Alifafanua kuwa Milinga inadaiwa alichomwa na chupa hiyo shingoni na kusababisha kutokwa damu nyingi ambazo ndizo zilimsababishia kifo na kwamba chanzo cha ugomvi ilikuwa ni wivu wa mapenzi na inadaiwa muda mchache kabla ya tukio hilo Milinga alipata taarifa kutoka kwa wanakijiji wenzake kuwa mke wake ambaye jina lake limehifadhiwa alikuwa na mwanamke ambaye ni rafiki yake walikuwa wanakunywa pombe na askari wawili wa jeshi la kujenga taifa ndani ya eneo linalouzwa pombe (bia).

Alisema baada ya mtuhumiwa Milinga kufuatilia taarifa aliyokuwa ameipata kutoka kwa wanakijiji wenzake ghafla aliwakuta mke wake pamoja na rafiki yake mwanamke wakiwa na askari wawili wa kiume wa jeshi la kujenga taifa wakiwa wanakunywa pombe huku kila mwanamke alikuwa na mwanaume wake na mke wa mtuhumiwa Milinga alikuwa amekaa na askari mwanafunzi Haule huku akiwa ameshika simu ya Haule kitendo ambacho kilimuudhi mtuhumiwa Milinga.

Alibainisha zaidi kuwa inadaiwa kuwa mtuhumiwa baada ya kuwakuta kwenye eneo la tukio hilo ndipo alipoanza kumpiga mke wake na baadae alimjeruhi Haule shingoni kwa kutumia chupa ya soda ambayo alikuwa ameivunja na kumsababishia kifo papo hapo baada ya kuvuja damu nyingi.

Hata hivyo kaimu kamanda Chiposi alieleza kuwa mtuhumiwa milinga baada ya tukio hilo kutokea na kugundua kuwa ameua alikimbia na kutokomea kusikojulikana na jeshi la polisi linaendelea kumsaka
Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top