MWENDESHA pikipiki Dastan Mbena
(30) mkazi wa Songea mjini anashikiliwa na polisi mkoani Ruvuma akikabiliwa na
tuhuma za kukutwa na risasi saba zinazodaiwa kuwa ni za bunduki aina ya Riffle
ambazo alikuwa amezibeba kwenye mfuko uliofungwa nyuma ya pikipiki aliyokuwa
akiendesha akitokea katika kijiji chA Namabengo wilayani Namtumbo kwenda Songea
mjini.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa
wa Ruvuma mrakibu mwandamizi wa polisi George Chiposi alisema kuwa tukio hilo
limetokea juzi majira ya saa nne asubuhi huko katika kijiji cha Mtwara pachani
kulichopo katika wilaya ya Namtumbo wakati akitokea namabengo kwenda Songea
mjini.
Kaimu kamanda Chiposi alifafanua
zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio askari polisi ambao walikuwa kwenye
doria kwa kazi maalum ambao waliongozwa na mkaguzi msaidizi wa polisi Adam
Kimbesi walimkamata Mbena baada ya kumkimbiza kwa muda mrefu akiwa kwenye
pikipiki yenye namba za usajili T536 BGX aina ya SanLg aliyokuwa akiiendesha.
Alisema kuwa askari hao baada ya
kufanikiwa kumkamata walimpekua na kukuta kwenye mfuko uliokuwa umefungwa nyuma
ya pikipiki hiyo ndani yake kulikuwa na risasi saba zinazotumika kwenye bunduki
aina ya riffle.
Hata hivyo kaimu kamanda chiposi
alisema kuwa mtuhumiwa amekamatwa na anatrajiwa kufikishwa mahakamani pindi
upelelezi wa tukio hilo utakapo kamilika.
Post a Comment