SACCOS ya walimu Songea mjini imepata Viongozi wapya baada ya kufanya uchaguzi ambapo
Gosberth Nchimbi ameibuka mshindi baada ya kupata kura 224 kati ya kura
281 zilizopigwa na kuwashindwa wenzake watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.
Akitangaza matokeo hayo jana wakati wa mkutano mkuu wa 15 wa wanachama wa saccos hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa Songea Club Msimamizi wa uchaguzi Kaimu afisa ushirika wa Manispaa Given Malick amemtangaza Gosberth Nchimbi kuwa ndiye mwenyekiti mpya baada ya mwenyekiti aliyekuwa akishikilia kiti hicho Martin Challe kutangaza kujihudhuru .
Amesema ,, kura zilizopigwa zilikuwa 281 na zilizoharibika ni kura 8 ambapo amewataja waliogombea nafasi ya mwenyekiti kuwa ni Gosbert Nchimbi
(224) Julie Luoga (27) Juliana Matembo (18) pamoja na Hilda Kapinga
(10) hivyo kwa nafasi hiyo Julie Luoga amechaguliwa kuwa Makamu
Mwenyekiti.
Amezitaja nafasi nyingine zilizogombewa kuwa ni mjumbe wa Bodi, imegombewa na Gosbert Nchimbi (212),Juliana Matembo (21),wengine ni Hilda kapinga (18) Regnbert Tindwa (17) pamoja na Salvatory Mhagama (7)
Aidha, anafsi ya mjumbe kura zilizopigwa ni 261 na zilizoharibika ni 44 ambapo wajumbe waliofanikiwa kushinda ni wanne
kati ya watano ambao walikuwa wakiwania kiti hicho ambapo
waliochaguliwa ni Julie Luoga,Salvina Kabanga,Timoth Ngonyani pamoja na
Benedict Mkinga,ambapo mgombea Isabela Henjewele hakmufanikiwa kupata nafasi hiyo.
Post a Comment