WATU
watatu wa familia moja wakazi wa kijiji cha Winga kilichopo katika
Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamejeruhiwa vibaya kwa kupigwa a radi
njee ya nyumba yao wakati wanakula chakula cha mchana baada ya kutoka
kwenye shughuli zao za shamba.
Kaimu kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mrakibu mwandamizi wa Polisi Gorge Chiposi amewataja
waliojeruhiwa kuwa ni Zainabu Ally (33),Ally Khamisi (5) na Hawa
Nigange (4)wote wakazi wa kijiji cha Rwinga nje kidogo ya mji wa
Namtumbo.
Kaimu
kamanda Chiposi alisema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 11
jioni huko katika kijiji cha Rwinga ambako watu watatu wa familia moja
wakiwa wanakula chakula nje ya nyumba yao ghafla mvua ya upepoe ambayo
iliambatana na radi ilianza kunyesha na baadae wakiwa wanaendele kula
chakula walipigwa na radi na kuwasababishia majeraha sehemu mbalimbali
ya mihili yao.
Alifafanua
kuwa inadaiwa Zainabu ambaye ni mama mzazi wa watoto hao alipigwa na
radi na kusababisha miguu yote miwili kupooza ,Mtoto Ally radi ilimbabua
maeneo ya paja la kushoto,tumboni na kwenye makalio yake na mtoto Hawa
alibabuliwa na radi mikononi na tumboni.
Alisema
kuwa majeruhi wote walikimbizwa katika hospitali ya serikali ya Wilaya
ya Namtumbo ambako wanaendelea kupata matibabu na hali zao bado sio
nzuri hata hivyo mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali
mkoani humo zimeharibu miundombinu ya barabara na kusababisha usafiri
kuwa mgumu.
Baadhi
ya wakazi wa manispaa ya Songea wamejikuta wakikosa huduma za mitandao
ya E-mail (barua pepe ) ambayo imesababisha huduma za ATM za taasisis za
kifedha zilizopo mkoani humo na barua pepe kutofanya kazi tangu Juzi
kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na radi kuharibu miundombinu
ya mawasilia
Post a Comment