JESHI la polisi mkoani Ruvuma
limemtia mbaroni Barnabas Chipeta (25) mkazi wa mahenge katika halmashauri ya
manispaa ya Songea kwa tuhuma za kusababisha kifo cha aliyekuwa abiria wake kwenye gari aliyokuwa akiiendesha
kutoka Songea kwenda Mbinga ambayo ikiwa kwenye mwendo mkali iliacha njia na
kupinduka.
Akizungumza ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi
mrakibu mwandamizi wa polisi George Chiposi
alisema kuwa tukio hio lilitokea juzi majira ya saa tatu usiku huko
katika kijiji cha Liganga wilaya ya Songea vijijini.
Kaimu kamanda Chiposi alibainisha
zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio kwenye barabara itokayo Songea kwenda
Mbinga gari lenye namba za usajili T104
ANM aina ya Mitsubishi Canter iliyokuwa ikiendeshwa na Chipeta ikiwa kwenye
mwendo mkali ikitokea Songea kwenda Mbinga iliacha njia na kupinduka na
kusababisha kifo cha Iddi Said(25) mkazi wa madizini manispaa ya Songea.
Alisema kuwa dereva Chipeta akiwa
na abiria huku akitambua kuwa anavunja sheria aliendesha gari kwa mwendo kasi
ambaoulimsababishia ashindwe kabisa kuumudu usukani jambo ambalo lilimfanya
apate ajali hiyo ambapo abiria wake Iddi Said alifariki papo hapo.
Alieleza kuwa chanzo ni mwendo
kasi ambao pia ulisababisha magurudumu ya mbele ya gari hiyo kupasuka baada ya
kutokea ajali na kwamba dereva wa gari hiyo wakati anafanya jitihada za kutaka
kukimbia wananchi wa kijiji hicho walimkamata na kwa sasa yupo mikononi mwa
polisi na upelelezi zaidi wa tukio hilo unafanywa na utakapokamiliza atafikishwa
mahakamani kujibu shitaka hilo.
Post a Comment