|
WATU
watano wamefariki dunia mkoani Mbeya kwa kupigwa radi katika matukio matatu
tofauti likiwemo lililoua ndugu watatu wa familia moja. Wanandugu hao watatu
wakazi wa kata ya Nyimbili wilayani Mbozi wamefikwa na mauti Februari 5 mwaka
huu majira ya saa saba mchana wakati mvua kubwa iliyoambatana na radi za mara
kwa mara ikiendelea kunyesha wakiwa nyumbani.
Afisa
mtendaji wa kata ya Nyimbili Lingtone Nzowa amewataja waliopoteza maisha kuwa
ni Jerumana Halinga(35),David Halinga(5) na Kumi Halinga(3) ambapo pia radi
hiyo imemjeruhi mtoto wa miezi tisa ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Tukio
la pili limetokea katika kijiji cha Magurula kata ya Utengule Usangu Wilayani
Mbarali ambapo radi iliyotokana na mvua kubwa imempiga Kasim Sagutangu na
kusababisha kifo chake ambapo diwani wa kata hiyo Juntwa Mwalyaje amesema mvua
hiyo imenyesha Februari 3 majira ya saa nane za mchana.
Tukio
la tatu limetokea februari 3 katika kijiji cha Mbagala Kata ya Ilembo wilayani
Mbeya ambapo mwanamke Kotanida Petro amefariki dunia baada ya kupigwa na radi
akiwa shambani kwake.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio
hayo ya vifo vya watu watano vilivyotokana na radi.
|
Tuesday, February 5, 2013
Post a Comment