Wajumbe wa kuandaa rasimu ya katiba mpya Tanzania
Sifa za Watakaochaguliwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, Ngazi ya Serikali za Mitaa
Wajumbe wanne kutoka kila Kata kwa Tanzania Bara na wanane kutoka kila
Kata katika Mkoa wa Dar es Salaam na Wajumbe watatu kutoka kila Shehia
kwa Zanzibar wanapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
1.1.Awe Raia wa Tanzania.
1.2.Awe na umri wa miaka 18 au zaidi.
1.3.Awe na uwezo wa kusoma na kuandika.
1.4.Awe mkazi wa kudumu wa Kijiji/ Mtaa / Shehia husika.
1.5.Awe Mtu mwenye hekima, busara na uadilifu.
1.6.Awe Mtu mwenye uwezo wa kujieleza na kupambanua mambo.
MAMBO YA KUZINGATIWA
Utaratibu wa kuwapata Wajumbe kwa Tanzania Bara na Zanzibar uzingatie mambo yafuatayo:-
2.1.Uwakilishi wa watu wazima.
2.2.Uwakilishi wa wanawake.
2.3.Uwakilishi wa vijana.
2.4.Jiografia ya Kata/ Wadi / Kijiji / Mtaa / Shehia husika
Loading...
Post a Comment