Loading...

BREAKING NEWS: Mauaji ya Askari Mkoani Ruvuma

Wananchi na waendesha bodaboda wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wamemuua askari polisi baada ya mwendesha boda boda mwenzao kuuliwa na askari polisi.

Mwendesha boda boda huyo aliyeuliwa inasemekana ni wale wavunjaji wa sheria za barabarani, baada ya kufanya kosa la kuvunja sheria walikimbizana na askari polisi na ndipo askari polisi alipoachia risasi iliyomuua dereva boda boda huyo.

Baada ya tukio hilo waendesha boda boda wa eneo hilo kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi walianza mashambulizi ya silaha za jadi dhidi ya askari hao na hatimaye kumuua askari mmoja.
HABARI ZAIDI TUTAWALETEA HAPA HAPA songeayetu.blogspot.comPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top