Loading...

KANISA LAFUNGUKA VURUGU ZINAZOENDELEA NCHINI

KANISA limesema kuwa kama Serikali itaendelea kushindwa kuchukua hatua za kuwalinda wananchi wake na kuwatendea kwa usawa bila ya ubaguzi kwa mujibu wa ibara ya 12 na 13 ya Katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  kanisa litachukua hatua kwa kuwaaeleza waumini wake kwa uwazi kuwa Serikali iliyopo madarakani inaibeba Dini moja

Hayo yalisemwa na Katibu wa umoja wa Makanisa Kikrsto Wilaya ya Tunduru Padre Dominiki Mkapa wakati akiwasomea waumini wake Waraka wa Tamko lililotolewa hivi karibuni na Jukwa la Wakristo Tanzania (TCF) na kusambazwa katika Makanisa yote nchini na kuongeza kuwa baada ya kufikia maamuzi hayo pia Kanisa litatafakari upya juu ya mahusiano kati yake na Serikali.

Waraka huo uliotisa saini na Mwenyekiti wa Umoja huo (CCT) Askofu Peter Kitula Machi 19 mwaka huu ambao mtandao huu umefanikiwa kuuona   na kuipata nakala yake unafafanua kuwa hatua hiyo imetokana na Serikali kutochukua hatua madhubuti kwa watu wanaobainika wazi wazi kutumia mwamvuli wa Dini kufanya vitendo vibaya yakiwemo mauaji na vitisho kwa viongozi wa Dini nyingine na kuivuluga amani na utulivu wa taifa letu.

Aidha waraka huo uliendelea kueleza kuwa kutokana na udhaifu huo wa Serikali kuendelea kufumbia macho vitendo hivyo kikundi hicho kimekuwa kikiendeleza utekelezaji wa matukio hayo hali inayolishawishi Kanisa kufikilia vinginevyo likiwemo wazo la kutamani kuutangazia kuwa hivi sasa Tanzania ni nchi inayovunja haki za Binadamu kwa ubaguzi wa dini na kulitesa Kanisa kimfumo.

Awali Askofu wa Jimbo kuu la TUNDURU/Masasi Mhashamu Castory Msemwa aliwahimiza wazazi na walezi kuwasaidia wachungaji katika malezi ya Watoto wao zikiwa ni juhudi za kuwalea katika maadili mema na kuongeza kuwa vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyotekelezwa sasa vinatokana na kuporomoka kwa maadili.

Askofu Msemwa ambaye alikuwa akiongea na waumini wake katika kanisa Katoliki kupitia mahubiri aliyo yatoa wakati wa ibada ya maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka taliyofanyika katika kanisa la Mtakatiofu mathias Mulumba Kalemba mjini Tunduru Mkoani Ruvuma na kuongeza kuwa Watoto wasipo lelewa na kupewa elimu ya kutosho katika maadili na misingi mikuu ya imani ya Dini husika ipo hatari kwa watoto hao kuingia katika mikumbo mibaya hali itakayo wasukuma kutotenda mema katika jamii.

Pamoja kutolea mifano ya matukio yanayotishia kuvunjika kwa amani na utulivu wa taifa la Tanzania yaliyoibika hivi karibuni, Askofu Msemwa aliwataka waumini wake kusimamia imani yao kikamilifu na kuto waogopa wauaji hao wanaotishia imani za wengine kwa madai kuwa wanacho weza kukitoa uhai ni mwili tu lakini Roho itabaki hai.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top